Staa wa sinema na muziki Bongo, Snura Anton Mushi na
Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa wamenaswa ‘laivu’ wakiwa
kimahaba......
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, tukio hilo lililijiri
hivi karibuni nyumbani kwa Snura maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam
ambapo wawili hao walibambwa wakiwa wamejiachia ‘wakifanya yao’.
Mnyetishaji huyo alidai kuwa wawili hao walikuwa
wakiminyana bila kujali macho ya watu waliokuwa wakifika nyumbani kwa Snura
hasa marafiki na majirani zake.
“Yaani walikuwa wakioneshana mahaba kama njiwa bila kificho chochote.
“Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.
“Yaani walikuwa wakioneshana mahaba kama njiwa bila kificho chochote.
“Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.
“Baadaye hata Ngassa naye alifanya hivyohivyo huku
akicheza na nywele za Snura anavyotaka,” alidai shuhuda wetu.
Ili kujiridhisha, Tulisaka picha za wawili hao ambazo
walikuwa ‘wakijifotoa’ kwa simu zikiwaonesha wakiwa katika mahaba jambo
lililozua utata na maswali kwa walioziona.
Uchunguzi ulibainisha kuwa siyo mara ya kwanza kwa Snura
na Ngassa kunaswa wakiwa beneti kwani wiki mbili zilizopita walibambwa kwenye
ukumbi mmoja wa starehe jijini Dar wakila bata ndefu.
Baada ya kulishwa ‘niuzi’ hizo,Tulimsaka Snura ambapo
alipopatikana alitakiwa alimwagiwa habari yote juu ya uhusiano wake tata na
Ngassa ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nimeshtuka sana kusikia hizo picha zimewafikia kwa
sababu mimi na Ngassa ni marafiki na yeye (Ngassa) ni shabiki mkubwa wa nyimbo
zangu.
Ngassa na Snura ndani ya pozi tata.
“Ngassa alinitembelea kama marafiki wengine wanaokuja
nyumbani kwangu. Simu yangu ilipotea ndiyo maana picha zikavuja lakini ukweli
ndiyo huo.”
Kwa upande wake Ngassa ambaye yupo mapumzikoni baada ya
kumalizika kwa msimu wa kwanza wa Ligi Kuu Bara hakuweza kusema chochote
kufuatia simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.


No comments:
Post a Comment