
Akizungumza na mwandishi wetu jana
katika usiku wa Red Ribbon Fashion Galla iliyofanyika Mlimani City jijini Dar
es Salaam, Lulu alisema siku ya Ukimwi duniani inatukumbusha kuangalia tumetoka
wapi na tunakwenda wapi na kuangalia wangapi wamepoteza maisha kwaajili ya gonjwa
la Ukimwi.
“Najumuika na Watanzania leo ,siku ya
Ukimwi duniani ambayo hufanyika kila mwaka, kwa kuangalia wangapi wamepoteza
maisha, pamoja na kuwahamasisha zaidi vijana Wakitanzania kutumia kinga ili
kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi ambavyo vinapoteza nguvu ya Taifa,”
alisema Lulu.
Pia Lulu alisema amekuwa akipima
Ukimwi mara kwa mara ili kuangalia afya yake,huku akiwashauri vijana kwenda
kupima ili kujua afya zao.
“Nimekuwa nikipima HIV kila mara
katika hatua za maisha yangu,kuangalia kuhakikisha najiweka katika usalama wa
afya yangu,pamoja na kupanga matarajio ya maisha.Sio kuwa ukipima
ukagundulikana una HIV utashindwa kupanga malengo yako hapana! ukipata ushauri
nasaha, ukajua uishi vipi kwa kuboresha afya yako, maisha yataendelea kama
kawaida. Kwahiyo kinachotakiwa vijana ni kujua afya zetu mapema”
No comments:
Post a Comment