.jpg)
MODO mwenye mvuto Bongo
Jacqueline Patrick ‘Jack’, ambaye yuko mahabusu ya Gereza la Qincheng nchini
China kwa madai ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini humo, anazidi kuteseka,
safari hii akidaiwa kukabiliwa na tatizo kubwa la kiafya.Kwa mujibu wa chanzo
chetu, Jack anasumbuliwa na ugonjwa wa kukosa hamu ya kula, hali iliyomfanya
apoteze uzito wa kilo kumi huku akikabiliwa na tatizo lingine la kupungua kwa
kasi ya mapigo ya moyo.
KAMA HALI ITAENDELEA
Chanzo kimesema kuwa endapo hali ya kuzorota kwa afya hiyo kutaendelea, Jack anaweza kujikuta katika tatizo kubwa zaidi ambalo linaweza kusumbua kwenye mwenendo mzima wa kesi yake.

“Kusema kweli kuhusu maisha ya mahabusu si mabaya sana
kwake, hateswi kwa kupigwa wala hanyimwi chakula, ila hana uhuru binafsi, ni
kama amefichwa, naamini matatizo hayo ya kiafya yanatokana na uzito wa kesi
yake,” kilisema chanzo hicho.
MLOLONGO WA MAMBO
Habari zaidi zinadai kwamba kesi ya msingi ya staa huyo kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya itaanza kusikilizwa rasmi Septemba, mwaka huu baada ya mwanasheria wake kukamilisha taratibu zote.
“Ile kesi yake sasa ni Septemba mwaka huu. Si unajua hajawahi kupandishwa kizimbani kuulizwa kama ni kweli alikamatwa na unga au la!” kilisema chanzo hicho.

WAKILI
WAKE ANATOKA HONG KONG
Taarifa zaidi zinasema kuwa wakili wa mrembo huyo anatoka jijini Hong Kong nchini humo ambako ndiko kwenye wanasheria wazuri kwa kiwango cha kesi yake ya unga.
KUMWONA NI KWA AHADI
Ikazidi kudaiwa kwamba kuna Mtanzania mmoja tu ambaye amekuwa na fursa ya kumuona modo huyo na kabla ya kwenda lazima aombe na kupewa ‘apointimenti’ maalum.
WALIOMTUMA WAMPIGA CHENGA, WALA ‘BATA’ Tofauti na kwa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye naye aliwahi kupata msala mkubwa kama huo nchini Afrika Kusini, Julai, mwaka jana ambapo ‘mabosi’ wake walikuwa mstari wa mbele kumhangaikia, Jack anasota mwenyewe.

Juzi, Risasi Mchanganyiko lilizungumza na mtu wa karibu sana na mtuhumiwa huyo
ambapo alikiri Jack kuwa na hali ngumu katika kesi yake hiyo huku akisema
kwamba watu wanaodaiwa ndiyo mabosi wake wanakula ‘bata’ tu jijini Dar es
Salaam.
“Unajua tatizo la biashara ya unga ni hapo tu! Wewe unayebeba ukinaswa ni juu yako, waliokutuma wao wanachofanya ni kuthibitisha tu kuwa ni kweli umekamatwa maana wapo wanaodaiwa wamekamatwa kumbe si kweli, wanaingia mitini na mzigo,” alisema mtu huyo.

TUKUMBUKE
Mrembo huyo alikamatwa Desemba 19, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Macau, China akitokea Bangkok, Thailand akiwa na kete 57 (kilo 1.1) za heroin tumboni zikiwa na thamani ya jumla ya zaidi ya shilingi milioni 300.
Awali ilidaiwa kuwa kesi yake ingeanza kusikilizwa mwaka 2016 baada ya yeye kujifunza Kireno (lugha inayotumika Macau) kwa miaka miwili.

No comments:
Post a Comment