Mtoto
Anastazia Jumanne akiwa amefungwa mikono yake kwenye pikipiki kwa mpira.
Mtoto Anastazia Jumanne (12) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi katika wilaya na mkoa wa Geita amefanyiwa ukatili wa kutisha baada kufungwa mpira kwenye pikipiki na baba yake mzazi na kisha kuanza kumburuza mtaani.

Tukio
hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya saa tatu asubuhi katika moja ya
mitaa ya mjini humo ambapo inadaiwa kuwa binti huyo anayesoma darasa la nne
katika shule hiyo alikataa kwenda shule kitendo ambacho kilimkasirisha baba
yake aitwaye Jumanne Nkoyogi ambaye pia ni mfanyabiashara wa samaki mjini
Geita.
Mashuhuda
wa tukio hilo baada ya kuona asubuhi hiyo mtoto huyo akiburuzwa huku amefungwa
kwenye pikipiki walianza kupiga makelele na kukusanyana kwa lengo la kumkamata
baba huyo aliyekuwa anafanya unyama huo.
No comments:
Post a Comment