Visitors


hit counter

Breaking News

728-banner


web counter

OnAir

Tuesday, 25 March 2014

HATIMAE WASHIRIKI 29 WA MAISHA PLUS WAINGIA KIJIJINI, KUSHINDANIA TSH MILION 25

Washiriki wa shindano la Mshindi wa Maisha Plus wakipewa maelekezo machache mara baada ya kuwasili kijijini kwao.
Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) akiongea katka uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus, ambapo jana washiriki wapatao 29 waliingia kijijini kuanza kukabiliana na changamoto za kuweza kupata shilingi milioni 25 za kitanzania.


Wageni waalikwa waliofika kijijini cha Maisha Plus kuangalia uzinduzi...

Mmoja ya wawakilishi toka Oxfam ambao ni wadhamnini wa Maisha Plus 2014 akizungumza machache. Pembeni yake ni Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya).

Mkuu wa Kijiji... Mwite babu wa kaya akiwepo kuhakikisha wanakijiji wanakaribishwa kwa shangwe.

Wageni waalikwa. 

Kazi ya kujenga nyumba za kuishi washirki wa maisha plus ikiendelea... ambapo washiriki hao walitakiwa kujenga nyumba zao za kuishi ndani ya masaa 48. 

Kila mmoja anawajibika kuhakikisha kazi ya kujenga nyumba inafanikiwa

Wadau kutoka Oxfam wakibadilisha mawazo mara baada ya kufika katika tukio la uzinduzi wa wawashiriki kuingia kijijini.

kuelekea kijiji cha Maisha Plus imeanza rasmi... washiriki wakiwa wamebeba mabegi yao ambapo kila mmoja alibeba mzigo wake mwenyewe kwa kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 1.5.

Safari ikiendelea huku washiriki wakiwa wameshachoka... wengine walitamani kughairi kuendelea na safari.

Wengine ilibidi wasaidiane kupeba mizigo.

Hakuna kuchoka, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe...

Wengine waliamua kulala ili waweze kunyoosha mgongo.

Read more ...

BREAKING NEWS:MKUU WA MKOA WA MARA, GABRIEL TUPPA AFARIKI DUNIA

Mkuu wa mkoa wa Mara, Bw. John Gabriel Tuppa.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Bw. John Gabriel Tuppa.
MKUU wa mkoa wa Mara, Bw. John Gabriel Tuppa, amefariki dunia ghafla leo majira ya saa 4.30 asubuhi baada ya kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa shinikizo la damu akiwa wilaya ya Tarime mkoani Mara.
Katibu tawala wa mkoa wa Mara, Bw. Benedict Ole Kuyan, amesema kuwa Bw. Tuppa kabla ya kifo chake leo asubuhi akiwa na afya njema alifika katika ofisi ya za mkoa na kumuaga kuwa anakwenda kufunga mafunzo ya mgambo katika kijiji cha Nyamwaga wilayani Tarime.
Amesema kuwa muda mfupi baada ya kufika katika ofisi ya mkuu wa wilaya, alipatwa na tatizo la ugonjwa huo na muda mfupi alikimbizwa hospitali ya Tarime lakini alifariki wakati akipatiwa matibabu.
Katibu tawala huyo amesema mwili wa marehemu unasafarishwa kutoka Tarime kuja hospitali ya Musoma kwa ajili ya kuhifadhiwa wakati taratibu nyingine na maelekezo ya kiserikali yakisubiriwa kutolewa.
Read more ...

SITTA HUU NDIYO WAKATI MUAFAKA

Sitta

Baada ya kusema hayo, niwashukuru sana Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Jaji Joseph Sinde Warioba kwa hotuba zao nzuri walizozitoa mbele ya Bunge Maalum la Katiba, wakati wa uwasilishwaji wa rasimu na uzinduzi rasmi wa chombo hicho.
Hakika, lilikuwa ni jambo la kufurahisha sana kuwaona viongozi hao wakitoa hotuba ambazo ziliwavutia sana watu waliozisikiliza, kwani kila mmoja alijenga hoja kwa umahiri wa hali ya juu, kiasi cha wananchi kuzidi kuchanganyikiwa kuhusu mustakabali wa taifa letu, hasa kwa masuala nyeti kama yale yanayohusu muungano wetu.
Kwa maoni yangu, wote wawili walikuwa na hoja kwa wanachokiamini, kilichobaki ni kuwaachia wajumbe wa Bunge Maalum kuchuja pumba na mchele, ili Mtanzania ale wali safi usio na chenga.
Read more ...

SOMA POST YA JOTI KATIKA PAGE YAKE YA FACEBOOK


Nasema hivi, nawaangalia mnavyoandika hiyo Katiba. Mkizingua wote mnakula bakora.

Read more ...

AIBUU..!! DENTI WA CHUO AFAKAMIA POMBE NA KUMTIA AIBU ..JIONEE PICHA HAPA

Huyu ni denti wa chuo kimoja hapa Town, in the name of kula bata alijikuta akifanya mambo ya ajabu....Thanks kwa watu walio mrudisha hostel.....Dada zetu pombe sio chai....



Read more ...

MASIKINI BELE 9 CHUPUCHUPU KUIONJA JELA, KISA ATAKA KUTAKA KUMTAPELI PROMOTA. MKASA MZIMA HUU HAPA


Belle 9
Inasemekana Eti Mwanzoni mwa mwezi huu mkali wa RnB Belle 9 nusura ainuse jela baada ya kuchukua pesa za mapromota wawili wa Mafinga Iringa ambapo walikua wanashow katika weekend moja na Belle 9 akaamua kutumbuiza show moja na kumtosa promota mmoja kwa madai kuwa anatakiwa kuendelea kui promote show hiyo, sasa promota aliyetoswa hakujua kama Belle 9 atakuja kuperform katika mji wake lakini alipokuja kushtukia ndio akaamua kwenda katika ukumbi huo Belle 9 alipomaliza kutumbuiza wakamkamata na kumpeleka kituo cha polisi ndo ikaamuliwa kuwa kesho yake Belle 9 apige show ili kuepuka utata huo,
skiza You Heard Ilivyokua kwenye XXL ya Clouds fm - 


Read more ...

ANGALIA VIDEO MPYA YA SHILOLE -CHUNA BUZI


Video hii imetoka ila hii ni kwa ajili ya Mitandao tu kwani humo ndani ni maono matupu ..yakuonekana kwenye Tv itafuata soon.....Angalia hapa ujionee mwenyewe Buzi linavyochunwa 


Read more ...

DIAMOND PLATINUM AFUNGUKA KWA KUSEMA BAADA YA VIJANA WAKE KUPATA WATOTO SASA NI ZAMU YAKE YEYE KUPATA MTOTO

diamondplatnumzLeo tulikuwa tunamtoa mtoto wetu mwingine toka kwa bwana #Moze_Iyobo na bi #Mwengi.... Eeh! Mwenyezi Mungu, wajaalie na hawa vijana wawili walio baki @emma_platnum na @tonser66wamalize haraka nao, ili Mtu mzima sasa nianze kufyatua copy zangu ��.. �������� au mda wangu Bado??
Read more ...

COMMENT YA MASANJA MKANDAMIZAJI FACEBOOK


Wife material saa hii yuko home ananyoosha nguo alizofua jana na kujiandaa kwa ajili ya shughuli za kesho. Sio anachambua mitaa huku amepaka milipustiki utadhani fisi amekunywa damu
Read more ...

RAY C NA MPANGO WA KUNYAKUA PENZI LA DIAMOND PLATNUMZ KUTOKA WA WEMA...CHEKI HAPA


Msanii "kiuno bila mfupa" Rehema Chalamila. 'Ray C' anadaiwa kuwa bize na harakati za kumnasa sukari ya warembo Naseeb Abdul 'Diamond' katika anga za maoenzi huku duru za habari zikidai kuwa muda si mrefu kuanzia saaa yataandikwa mengi juu ya wawili hao


Mwandishi wetu alizungumza na rafiki wa karibu na Ray C hivi karibuni na kuambiwa kuwa muda mwingi jina la Diamond halikatiki mdomoni mwa mrembo huyo.
Diamond Platnumz

 Chanzo chetu cha habari kilizidi kudai kuwa kwa sasa Ray C hana furaha hadi atakapotimiza nia na lengo la kumnasa Diamond hapo ndipo furaha yake itakapotimu

Aidha habari zinazidi kudai kuwa mara kadhaa Ray C amekuwa akipanga Miadi ya kukutana na Diamond licha yakushindikana kwa apointiment hizo kila mara "kwasasa Ray C haambiwi kitu kwa Diamond, ana haha kila wakati kumweka mikononi mwake, hana furaha kabisa hadi lengo lake litakapotimia, na muda si mrefu mtaandika juu ya hao" alisema rafiki ea Karibu na Ray C
Wema Sepetu
Mwandishi wetu aliwatafuta wawili hao kwa njia ya simu ambapo simu ya Ray C ilionekana kuwa bize muda mwingi huku Diamond akidai kutokuwa na taarifa juu ya madai hao "kaka mimi sina taarifa kabisa na habari hizo, kwangu Ray C namchukulia kama dada yangu" alisema Diamond.
Mwandishi wetu alipomtaka Diamond kufafanua hatua atakayochukua endapo mrembo huyo ataamua kumwambia anamtaka ambapo kwa haraka Diamond alisema "NO COMNENT (sina cha kujibu)"  na kukata simu.



Read more ...

PADRI AKUTA TUNGULI KABURINI KWA NGWEA

Ooo…Nooo! Wakati hati ya kifo cha aliyekuwa rapa bora Bongo, marehemu Albert Keneth Mangweha ‘Ngwea’, ikiendelea kushikiliwa nchini Afrika Kusini alikokutwa na umauti mwaka jana, kwenye kaburi lake kumekutwa tunguli zilizozungushiwa sanda,Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.

PADRI AKEMEA
Awali, ilielezwa kuwa siku hiyo padri huyo alioteshwa ndoto usiku juu ya uwepo wa vitu vya ajabu katika makaburi hayo ndipo akakemea kabla ya kwenda kuvishuhudia asubuhi yake (Ijumaa iliyopita) huku paparazi wetu akinyetishiwa na kuwahi eneo la tukio.
PAPARAZI USO KWA USO NA PADRI
Paparazi wetu alipofika eneo la tukio alikutana uso kwa uso na kiongozi huyo wa kiroho akiwa amesimama kwenye kaburi hilo la Ngwea.
Paparazi wetu alipomfikia Padri huyo alimuuliza kulikoni ndipo alipomsimulia kisa kizima.
“Jana (Alhamisi ya wiki iliyopita) nilioteshwa juu ya kuwepo kwa vitu vibaya kwenye makaburi haya ya waumini wetu ambayo yapo nje ya kanisa letu.
“Nilishtuka sana na kuona mambo ya ajabu, nikaamua kushusha maombi ya kukemea ambapo nilioteshwa kuwepo kwa vitu kwenye makaburi yetu ambayo yako jirani kabisa na sehemu ninayo lala,” alisema Padri Msimbe na kuongeza:


“Leo kulipokucha ndipo nikafika kwenye makaburi haya na kuanza kukagua yote likiwemo la Mangweha (Ngwea) nikayakuta yakiwa na tunguli zilizovishwa sanda ambazo pia zina majina ya waumini wangu wa moja ya vigango vya parokia hii.”

AKATAA KUTAJA MAJINA
Alipoombwa kutaja majina ya waumini hao alisema: “Sitaweza kutaja majina yao wala ya kigango yaliyoandikwa kwani wanajijua wenyewe na mbaya zaidi hata waumini wataona katika ibada Jumapili hii (Jumapili iliyopita), nitaonesha madhabahuni,” alisema padri huyo ambaye tangu alipofika kwenye kanisani hilo limekuwa na maendeleo makubwa.
Kama alivyoahidi, ilipofika Jumapili iliyopita, padri huyo akiwa madhabahuni alisitisha mahubiri kisha akatoa tunguli hizo na sanda na kuwaonesha waumini.
Aliwatangazia waumini hao kuwa vitu hivyo alivikuta kwenye kaburi hilo ambapo alisema kuwa sanda hizo zilikuwa zimeandikwa majina ya baadhi ya wafuasi wa kanisa hilo ndipo kukaibuka hofu hivyo ikabidi maombi ya nguvu yafanyike.
Pamoja na maombi ya nguvu lakini walioona majina ya baadhi waumini wenzao kwenye sanda hizo, walianza kushikwa na mshangao huku wakitazamana usoni.
Paparazi wetu alifikia kwenye ibada hiyo na kujionea jinsi waumini walivyotaharuki kutokana na vitendo hivyo ambavyo vilitokea katika makaburi hayo.
“Mimi hata sielewi maana kwa jinsi ninavyoona, itakuwa kuna watu wasio na hofu ya Mungu wanaendekeza mambo ya kishirikina, sasa wanaandika haya majina lakini najua kwa kuwa tumeyabaini, kwa nguvu za Mungu, watashindwa,” alisema muumini mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini.
Paparazi wetu alizidi kutafuta data zaidi juu ya sakata hilo ambapo mwishoni alijiridhisha kuwa tunguli hizo zilipokewa na waumini, zikahifadhiwa katika ofisi ya Padri Msimbe.
Mbali na tunguli hizo zilizokutwa katika kaburi la Ngwea, mwandishi wetu alijionea kiroba cha tunguli hizo zilizozungushiwa  sanda katika ofisi ya padri huyo zilizohifadhiwa chini ya meza.
Minong’ono zaidi ilizidi kuibuka kuwa huenda watu walioweka tunguli hizo kuwa wameweka katika kaburi la Ngwea ili waweze kung’ara kimuziki kama alivyokuwa marehemu.
“Watu wanadanganyana, wamesababisha waumini wengi kuingiwa na hofu juu ya nini hatma yao. Wanaamini mtu anaweza kufariki dunia na mwingine akatembelea nyota yake, tunapaswa kuishi katika matakwa ya kumuamini Mungu siku zote,” alisema muumini mwingine wa kanisa hilo ambaye ni kiongozi kanisani hapo.
Read more ...

KWANINI MAMBO HUWAENDEA MRAMA WASANII WANAO JITOA TIP-TOP CONNECTIONS?

Tip Top

Wako wapi MB Dog, Z-Anto, Keisha, Pingu, Spark, Dongo Janja na wengine waliowahi kujitoa Tip Top Connection? Kuna nini Tip Top, kwamba ukijiondoa tu huwezi kufanikiwa mbeleni? Kwanini ni wasanii wachache tu, tena anaweza kuwa Cassim Mganga peke yake ambaye baada ya kujiondoa kwenye himaya hiyo yenye makazi yake Manzese jijini Dar es Salaam, amefanikiwa kuwa na career ya kueleweka? Wengine wote, wamefeli.. big time.

Kinachosikitisha zaidi ni kuwa wengi wakiondoka hutoa maneno ya kashfa na hivyo kujikuta wakinyea kambi.

Hebu tuwaangalia hawa watatu, Dogo Janja, Z-Anto na MB Dog

Dogo Janja

Unakumbuka June 2012, kipindi Dogo Janja ameondoka Tip Top? Habari hiyo ilikuwa kubwa kiasi ambacho simu za Madee na Dogo Janja zilikuwa busy kwa interview. Kila pande ilikuwa ikiutupia lawama upande wa pili.

Kama umesahau wacha tukukumbushe ilivyokuwa.

Sababu zilizotajwa na Tip Top Connection ni kwamba Dogo Janja alilewa sifa na kuwa mtoro shuleni.
Kwa mujibu wa interview aliyofanya na Bongo5, uonevu na dhuluma ndivyo vilivyomchosha Dogo Janja kuishi Dar es Salaam na kujiondoa kwenye himaya hiyo.

Alisema tangu aje Dar es Salaam hakuwahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi kwake.

Alisema kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni moja. Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show. “Nilikuwa navumilia tu bro kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” aliiambia Bongo5.

Dogo alidai ilikuwa inafikia wakati akifanya show za ukumbuni hulipwa elfu hamsini au chini ya hapo na wakati mwingine alikuwa halipwi kabisa. Alisema tamaa ilizidi kumwingia Madee kiasi cha kumnyang’anya kadi yake ya benki na kuanza kuchukua hela bila kujua password aliipata wapi. “Kuna wakati nilikuwa nataka kumtumia mama laki moja, Madee akanikataza eti kwakuwa watadhani nina hela sana,” alisema.

Aliongeza kuwa kuna siku Madee alimpigia simu na kumwambia kuwa kaka yake wa Kibaha ameandaa show ya CCM na angemlipa shilingi laki moja. “Hivi kweli bro mimi ni mtu wa kufanya show ya laki moja?” alihoji. Hata hivyo aliamua kukubali ili kuepusha lawama.

Baada ya show kumalizika alisema yeye na back up artist wake walirudishwa saa saba usiku wakati asubuhi yake alitakiwa kwenda shuleni kuchukua namba ya mtihani na kuandaa dawati la kukalia. Dogo Janja alisema kuwa ilimuuma sana kwakuwa muziki haujampa chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati hata show kumtumia kimaslahi na hadi kufikia hatua ya kujenga nyumba yake.

“Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune,” alisema.

Alifunguka kuwa hadi kufikia Tip Top watangaze kumfukuza alikuwa kwa Tundaman akipiga story na Madee akamuita kisha kuanza kumpiga na kwamba alichukua simu yake akaondoka nayo. “Jamaa alianza kujitumia meseji kutoka kwenye simu yangu kwenda kwake za matusi ama kuwa nataka kumroga. Jana nimemuonesha Milard hizo meseji na amesikitika sana.”

Alisema kitendo cha kumwambia Madee kuwa amechoka na anataka kurudi nyumbani ndicho kilimfanya amfanyie yote hayo hadi kumwambia kuwa watahakikisha wanambania asifanye vizuri tena kwenye muziki. Pia amedai kuwa Madee aliwapigia simu wazazi wake ili wamkataze Dogo Janja asifanye interview na vyombo vya habari.

“Wanajua nikiongea wataabika sana.”

Baada ya drama zote hizo ndipo Ostaz Juma akaingia kwenye picha. Alimtumia nauli ya ndege rapper huyo kutoka Arusha kurejea Dar na akajiunga na Mtanashati Entertainment ambayo wakati huo ilikuwa na heshima kidogo. Dogo Janja alipewa maisha, akalipiwa ada ya shule na kutoa ngoma iitwayo Ya Moyoni aliyomshirikisha PNC. Haikupita muda, mambo yakaanza kutokota.

Kwa mara nyingi Ostaz Juma alimfukuza na kumrejesha tena rapper huyo kwa madai kuwa hakuwa na nidhamu. Hata hivyo, imefika wakati ambapo Mtanashati Entertainment imekosa muelekeo na Dogo Janja anahisi meli inazama. Kuomba msamaha ili mambo yaende ni kitu kisichoepukika kwake kwakuwa ni kweli Dogo Janja wa ‘Mtoto wa Uswazi’ ft Godzilla amepotea kabisa.

Z-Anto

Ni ngumu kuamini ukubwa wa Z-Anto baada ya kutoa hit single yake ‘Binti Kiziwi’ ungekuja kuyeyuka kama barafu ikutanapo na jua kali. Enzi Binti Kiziwi inahit, hakuna msanii aliyekuwa na show nyingi kama Z-Anto. Hata hivyo, meneja wa Tip Top Connection aliwahi kudai kuwa kipindi hiki ndipo msanii huyo alianza kuota ‘majipu’ kwapani na kuanza pozi nyingi. Jambo hilo lilimkera Babu Tale kiasi cha kuamua kuifuta kabisa video mpya ya msanii huyo iliyokuwa inategemewa kumpeleka juu zaidi. Baada ya kuondoka Tip Top mpaka leo hii, Z-Anto si yule tena wa zamani na ukweli hali yake kimuziki ni mbaya.

“Nililazimika kushuka kwa sababu hiyo. Lakini nilipokuja kuzigundua zile njia nikaweza kupenya na ngoma binafsi nilijisimamia mwenyewe kwa kila kitu ambayo ndio hiyo Kisiwa cha Malavidavi,” Z-Anto alikiambia kipindi cha Mseto cha Radio Citizen ya Kenya hivi karibuni japo alidai kuwa hadi leo Babu Tale anamtaka arejee kundini.

“Mpaka kesho (Babu Tale) bado ananipenda. Hata ukimuuliza katika wasanii wake anaowapenda atatajwa wawili asishindwe kunitaja mimi.”

MB Dogg

Unazikumbuza Latifa na Si Uliniambia? Hizo ni miongoni mwa nyimbo bora za Bongo Flava za muda wote lakini yuko wapi MB Dogg? Kama ilivyokuwa kwa Z-Anto, naye baada ya kujitoa Tip Top, mambo yalienda mrama. Ilimchukua miaka mingi MB Dogg kuweka ‘ego’ pembeni na kukubali kuwa kweli amepotea na anaiihitaji Tip Top kiasi cha mwaka huu kuweka mambo sawa na Babutale.

“Lakini kwa sasa nataka tumuangalie Mb Dogg kwa macho mawili,” Tale aliiambia Millaayo.com hivi karibuni. Mb Dogg ana kipaji watu wanaujua uwezo wa Mb Dogg, Mb Dogg sio kama amepotea hapana ila hana uongozi anahitaji promo ya nguvu tu akipata hiyo anarudi kupiga hela kama zamani.”

Hata yeye mwenyewe MB hivi karibuni alikiri kuwa kufanya muziki bila kuwa na uongozi wa kukusimamia ni kazi bure.

“Tip Top nilitoka na ndio kitu ambacho kilinirudisha nyuma sana,” MB Dogg aliiambia Bongo5 March 17 mwaka huu.

“Pale nilikuwa nafanyiwa kila kitu, nilikuwa narekodi tu kazi yangu vitu vingine vyote wanafanya wao so baada ya kutoka na kujisimamia mwenyewe nikaanza kuyumba na kuhangaika huku na kule. Kwahiyo kitu ambacho nimegundua msanii bila management nzuri huwezi fika mbali asikwambie mtu. Msanii anahitaji kuongozwa, kushauriwa na mambo mengine. Sasa hivi nipo Tip Top tumeingia makubaliano mapya ya kazi ndio maana nashukuru Mungu ngoma yetu mpya ‘Umenuna’ inasonga kidogo kidogo mpaka kieleweke.”

Kinachowaumiza zaidi wasanii walioondoka Tip Top ni kwamba wasanii waliosalia mathalani Madee, wameendelea kufanikiwa zaidi. Mwaka jana pekee, Madee anadai kuingiza zaidi ya shilingi milioni 150 kwa single yake moja tu ‘Sio Mimi’. Meneja wa Tip Top, Babu Tale akishirikiana na Said Fela ndio walio nyuma ya mafanikio ya Diamond Platnumz, kwahiyo ni wazi kuwa Babu Tale ni ‘hot cake’ kwa sasa na ndio maana wasanii wa Tip Top waliojiondoa wako radhi kumuomba msamaha ili warejee kundini.

Swali ninalokuacha nalo msomaji ni Je! Haiwezekani msanii aliyejiondoa Tip Top kuwa na career yenye mafanikio?

Read more ...

Sunday, 23 March 2014

DIAMOND AMEDATA NA KIPARA CHA WEMA

Wema

Diamond amefunguka hivi kwa kuweka picha hiyo hapo juu ya wema akiwa hana nywele yani kipara. Na kuandika Maneno haya: "So someone decided to go Bald...Lol! ��...what can i say, i love her either way...#Mahaba_niue #Kipara_ninyonge"
Baada ya Post hiyo naye wema sepetu aliweza kujibu kwa kuweka post yenye picha hii hapa na kusema hivi : “I just luv you Naseeb wangu”
hakika hawawatu wanapendana kwa kweli tungoje Ndoa tu sasa kilichobaki……
Team wema nao hawakuwa nyuma kusindikiza furaha hiyo ya hao wawili na waliweza kupost dongo hili likiwa na Picha hiyo hapo Juu, Daaaaahhh ni shida kweli……


Read more ...

Eti Mourinho alishangilia hivi kwenye chumba cha Wachezaji leo



Game ya leo ya Chelsea vs Arsenal imeisha kwa Chelsea kufunga ushindi wa goli sita kwa sifuri ambapo list ya wafungaji na mengine vipo kwenye post iliyopita.Wakati game hii ikiendelea Football Funnys ambao ni maarufu kwa kupost vituko mbalimbali kuhusu mchezo wa soccer, walipost video ya jamaa mmoja na kusema eti hivi ndivyo kocha wa Chelsea Mourinho alivyosherehekea ushindi wakati wa half time kwenye chumba cha Wachezaji.

Read more ...

DIAMOND AMEPOST UJUMBE HUU KATIKA PAGE YAKE YA FACEBOOK,SOMA HAPA

Morning Africa,...SIKU YA LEO UPATAPO NAFASI,HEBU JARIBU KUFANYA MOJA YA HAYA NA UTAKUWA UMEBADILISHA MAISHA YA MTU FLANI.
-Una mlinzi?instead ya kumfokea,Hebu leo kumbuka kumsalimu na kumtakia siku njema huytu mtu anayekesha getini kulinda nyumba yako,bila shaka wengi hawafanyi hili
1:shiriki bure sehemu ya chakula chako na yeyote mwenye njaa na kuhitaji
2:Shiriki nyimbo nzuri kwa mtu mwenye huzuni ama anye feel down
3:Mfundishe mtu ,jambo analotamani kulifaham na halifaham na ni wewe pekee unafahamu
4:Una nguo ama chochote usichokihitaji tena?hapana usikitupe,mpatie yule mwenye kuhitaji
5:Una rafiki ama jamaa mpweke na pengine hana mtu wa karibu wa kushare nae yanayomsibu,make a call am text kwake,mfanye ajiskie hayupo peke yake,kwani kuna siku nawe utakuwa mpweke na utatamani mtu wa kuzungumza nae
6:Panga ku donate damu,damu yako kidogo inaweza ikaokoa maisha ya mtu sehemu flani..
7:Saidia mzee,ama mtoto kuvuka barabara.
8:Ambia rafiki,family member ama mtumishi ni kiasi gani una mwappreciate
9:Saidia mji wako kuwa msafi,si kazi kubwa kuokota kipande cha uchafu na kuweka sehemu husika
10:Mpigie mzazi wako na kumwambia ni kiasi gani unampenda
11:Motivate mtu flani atimize ndoto zake
12:Jipe amani ya moyo kwa kusamehe
13: la mwisho,jifanyie wewe mwenyewe,Acha kufanya kitu kibaya ulichokuwa unaufanyia mwili wako,pengine uvutaji wa sigara,ulevi wa kupita kiasi etc
....HAIJALISHI NI KIDOGO KIASI GANI UTAKACHOKIFANYA,KUWEKA TABASAMU KWA MTU,NDICHO KINACHO MATTER ...Siku njema

Read more ...
Designed By Published.. Blogger Templates