Taarifa
ikufikie kutoka Samukawa, Kanagawa Japan ambako stori kwenye headlines ni
kampuni ya Nissan kupata furaha kubwa baada ya kufanikiwa kwa jaribio la gariwalilolitengeneza ambalo linajiendesha lenyewe. Unaambiwa
limetembea umbali wa kilometa 2.3 likijaribiwa kwenye mikikimikiki ya aina
mbalimbali barabarani kama vile kuovertake, kufata alama za barabarani, taa za
kuongozea magari na hata sehemu za watu kuvuka barabara.
Nissan wamesema wanalengo la kuanza
kuliuza hili gari miaka saba kutoka sasa, hiyo itakua mwaka 2020 ambapo gari
hili lina kamera maalum pamoja na sensors zinazofanikisha kulipa taarifa
ya tukio husika kwa wakati huo ndio maana linaweza kufanya kama inavyotakiwa
mfano kushika breki, kukanyaga mafuta na vitu vingine.
Kingine cha kushangaza, kwa mfano kwenye miji mikubwa ambayo parking ni tatizo unaweza kuliacha likajiendesha lenyewe kwenda kutafuta parking wakati wewe unawahi mahali alafu ukimaliza shughuli zako unalikuta linakusubiri likiwa limepaki vizuri kabisa.Baada ya kutazama hizo picha hapo juu, unaweza kutazama hii video kujiridhisha kikamilifu aisee japo hii video sio ya majaribio yaliyofanyika saa kadhaa zilizopita..

No comments:
Post a Comment