Visitors


hit counter

Breaking News

728-banner


web counter

OnAir

Friday, 29 November 2013

Maiti hufukuliwa makaburini ili kubadilishwa nguo huko Indonesia


Pichani ni baadhi ya wafu waliofukuliwa kaburini na kuvishwa nguo Indonesia.



KILA mwaka huko Tana Toraja, Indonesia, wafu (au maiti) hufukuliwa kutoka makaburini ili kubadilishwa nguo. Watu wa eneo hilo wa kabila la Toraja wana mila za ajabu kuhusu vifo na
maisha yanayofuata baada ya mtu kufa.

Wao mtu akifa hutakiwa kuzikwa katika eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia.
Idadi kubwa ya watu wa eneo hilo ni Wakristo, wanaofuata ni  Waislam  na wengine ni Wapagani ambao wanajulikana kwa imani  au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya Mababu”.

Torajan huishi katika maeneo ya milimani na hawataki kujulikana sana katika jamii, japokuwa wana mila na desturi zao zilizoenea katika jimbo la Sulawesi.

No comments:

Post a Comment

Designed By Published.. Blogger Templates