Muigizaji
na mwimbaji nchini Kitale yuko Tanga alipoenda kuhudhuria Dua ya kumuombea
marehemu Sharo Milionea ikiwa ni mwaka mmoja tangu afariki dunia kwa ajali
mbaya ya gari.
Kitale
ambaye ndiye msanii pekee aliyefika Tanga siku ya juzi amesema kuwa amejifunza
mambo mengi katika msiba wa rafiki yake Sharo Milionea, ikiwa ni pamoja na
misiba ya wasanii wengine waliotangulia mbele ya haki, Kanumba na Sajuki.
Akiongea
kwa njia ya simu na Edson Mkisi katika kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times
Fm, Kitale amesema kutokana na funzo alilopata ameampa ujumbe mama yake ili
kwamba pindi atakapotangulia mbele ya haki mambo hayo yasijirudie kwake.
“Nimejifunza
vitu vingi na nimejua marafiki walio wema na marafiki wasio wema. Ina maana
kwamba kuna marafiki wanafiki na marafiki wasio wanafiki. Amesema Kitale.
“Kuna
vitu vingi nimejifunza baada ya kuondoka marehemu Steven Kanumba, nimejifunza
baada ya kifo cha Sharo Milionea, na nimejifunza baada ya kifo cha Sajuki.
Nimejifunza vitu vingi sana sana sana.” Amesisitiza.
“Ina
maana hata mimi kama ntatangulia kuna mambo ambayo nimeshamweleza mama yangu na
nimeshaieleza familia yangu, nafikiri hakitakuja kutokea kama kilichotokea kwa
wenzangu. Nimejifunza vitu vingi hasa ukiwa msanii...” Kitale ameiambia Hatua
Tatu.
Hata
hivyo Kitale alikataa kueleza ujumbe huo na kudai kuwa ni siri kati yake na
familia yake kwa kuwa hafahamu nani atatangulia kati yake na wazazi wake.
Kitale
amewashauri wasanii kumkumbuka Mungu wakati wanapoendelea na shughuli zao na
ndio sababu watu wengi wanaamini kuwa asilimia kubwa ya wasanii ni ‘Freemason’,
na kwamba hiyo inatokana na kitendo cha wasanii hao kumsahamu Mungu wao.
(November 27,2012) ndio siku ambayo marehemu
Sharo Milionea alizikwa huko Tanga.
No comments:
Post a Comment