Msanii maarufu wa Marekani Kelly Rowland, ametinga uwanja
wa fisi Manzese Dar es salaam jana jioni baada ya kusikia sifa za
maeneo hayo ya Uswahilini tangu akiwa USA. Msanii huyo ametua
nchini kwa tiketi ya MTV kupitia taasisi yake inayojishughulisha na kampeni za
kupambana na Ukimwi (Staying Alive Foundation) ya
nchini Marekani, Kelly akiwa balozi wake. Akiwa Uwanja wa Fisi,
ambako kunasifika kwa ufuska wa kupindukia na rate kubwa ya maambukizi ya
virusi vya ukimwi kwa wasichana wadogo, Kelly alitembelea NGO ya EYG (Elizabeth
Youth Group) inayojishughulisha na kutoa misaada ya elimu ya HIV/AIDS,
uchangudoa, ulevi pamoja na uvutaji bangi kwa vijana nchini.
No comments:
Post a Comment