Wakati naendelea kuangalia funeral rites za Nelson Mandela, mliosikiliza hotuba ya JK ni kwamba kaeleza umati kwamba Mandela alifika Tanganyika kwa mara ya kwanza January 1962. Kwamba safari hiyo alikuja kisiri akipitia Mbeya na kuingia Tanganyika. Kisha akapewa passport ya Tanzania kusafiria. Hapa ndipo tunaposema viongozi wetu hawapekui vitabu au documents au hata kukumbuka tu. Ukweli ni kwamba historia haisemi hivyo.
Historia
inasema kwamba January 1962 ulikuwa ni mwezi mmoja tu tangu Tangayika ijitawale
ikiwa na Prime Minister Nyerere. Tukio kuu la kihistoria ni kwamba Huo mwezi
karibu wiki mbili zilitawaliwa na NEC ya TANU ambayo ilipomalizika Nyerere
akajiuzulu u-Prime Minister na akamuachia Rashid Kawawa. Gavana-General Richard
Turnbull asingeweza kutoa passport kwa Nelson Mandela kirahisi. Ukweli kuhusu
ujio wa Mandela ni kwamba alikuja hapa December 1962, yaani mwaka huohuo, na
akawepo kushuhudia Tanganyika ikipata status ya Republic. Hapo ndipo angeweza
kupata passport ya Tanganyika na ndicho kilichotokea. Sikuweza kuamini
Mheshimiwa JK alipokuwa anasoma zile tarehe mbele ya dunia nzima, kwa sababu
mtu aliyechimbua historia ya Mandela kokote ilikoandikwa anajua wazi kwamba
Mandela alikuja hapa December 1962. Na hata Mandela kwenye kitabu chake
alichoandika kiitwacho A LONG WALK TO
FREEDOM, ISBN: 9780349106533, pg.
345: {...we arrived in Dar Es Salaam the next day and I met Julius Nyerere,
the newly independent country's first President...} Hivyo, wakati ule
asingemkuta Nyerere akiwa President, na wakati pekee alipokuwa President ni
kuanzia December 09, 1962. KUSOMA KITU KABLA YA KWENDA PUBLIC NI MUHIMU.
Ni juzi tu miezi kadhaa iliyopita Naibu Waziri wa Elimu Mulugo aliwahi kusema
kuwa TANZANIA ni muungano wa nchi mbili TANGANYIKA NA ZIMBABWE. Hivi kweli
hata kama hotuba umeandaliwa, huwezi "kujiongeza". Ni shiiidah.
Credit
to: Sweetbert_Rwabukambara, Frudence & Fredrick kajuna
By: Tanzania
Nchi Yetu Sote.
No comments:
Post a Comment