Huenda
ukawa umejiuliza swali hili kwa kipindi kirefu lakini hujawahi kupata jibu.
Kwanini Tanzania, Afrika Kusini na Zambia zinatumia wimbo wa taifa wenye melody
inayofanana?
Melody
za wimbo huo ambao kwa Tanzania unaitwa ‘Mungu Ibariki Afrika, zimetoka kwenye
wimbo uitwao “Nkosi Sikelel’ iAfrika”, neno la lugha ya Xhosa lenye maana hiyo
hiyo pia). Wimbo huo ulitungwa mwaka 1897 na Enoch Sontonga,
aliyekuwa mwalimu kwenye shule ya misheni ya jijini Johannesburg.
Enoch
Sontonga
Wimbo huo ulianza kutumika kama wimbo
maalum wa hekaheka za ukombozi wa Afrika na baadaye kuanza kutumiwa kama nyimbo
za taifa za nchi tano barani Afrika, zikiwemo Zambia, Tanzania, Namibia na
Zimbabwe baada ya kupata uhuru.
Zimbabwe na Namibia zimepata nyimbo
zingine za taifa. Wimbo huo kwa sasa unatumika Tanzania, Zambia na tangu mwaka
1994 kama sehemu ya wimbo wa taifa wa Afrika Kusini.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa Tanzania
ndio ilikuwa nchi ya kwanza kuanza kuutumia wimbo huo kama wimbo wa taifa 1961
pale ilipokuwa Tanganyika na kuendelea nao baada ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar mwaka 1964
Tafsiri ya mashairi ya awali
yaliyokuwa kwa lugha Xhosa kwenda Kiswahili ilifanya na kundi la watu.
Wimbo unaotumiwa na Afrika Kusini
hata hivyo ni mchanganyiko wa “Nkosi Sikelel’ iAfrika” na “The Call of South
Africa” (unaojulikana kwa lugha ya Afrikaan kama “Die Stem van Suid Afrika”).
20 April, 1994 ndipo ilipotangazwa
kwamba zote Nkosi Sikelel’ iAfrika na Die Stem ziwe nyimbo za taifa za Afrika
Kusini. Wimbo uliounganishwa ulianza kufanya kazi October, 1997, baada ya
maneno ya Kiingereza yalipoongezwa na wimbo kupangwa upya na Jeanne Rudolph.
Chanzo: Bongo5
No comments:
Post a Comment