Nelson Mandela statue in South Africa |
Sanamu
hii ya Mandela iko mikono wazi ishara ya Mandela kukumbatia watu wa Afrika
Kusini Sanamu kubwa zaidi duniani ya Nelson Mandela imezinduliwa katika mji
mkuu wa Afrika kusini Pretoria siku moja baada ya rais huyo wa zamani kuzikwa.
Sanamu
hiyo iliyotengenezwa kwa shaba ina urefu wa mita tisa na ina uzani wa tani nne
unusu. Ilizinduliwa katika bustani la majengo ya bunge na inaonyesha Nelson
Mandela akihimiza umoja na maridhiano.
Sanamu
hiyo yenye mikono ya Mandela ikiwa wazi ilinuiwa kuonyesha Mandela
alivyoliungaisha taifa zima kwa mapenzi yake
Bwana
Mandela lipewa mazishi ya kitaifa nyumbani alikozaliwa katika kijiji cha Qunu
Jumapili
Familia
ya Madiba , viongozi wa ANC , viongozi wa Afrika na maafisa wengine wakuu
walihudhuria mazishi hayo katika kijiji cha Qunu mkoani Cape Mashariki
Kifo
cha Mandela kilifuatwa na maombolezi ya siku kumi na sherehe za kukumbuka
maisha ya Mandela aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95
Bendera
ya nchi hiyo ilirejeshwa kupepea katika urefu wake wa kaiwada.
Mandela
anakumbukwa kwa juhudi zake za kupatanisha wananchi na kupigia debe msamaha
miongoni mwa watu na ndio maana leo ikawa siku iliyotengwa kwa ajili ya
uzinduzi wa sanamu hiyo
Wakati
wa utawala wa wazungu, terehe 16 Disemba ilijulikana kama siku ya kuwakumbuka
mashujaa wa Afrikaners walioshinda vita dhidi ya jeshi la Zulu mwaka 1883.
Zaidi
ya karne moja baadaye mwaka 1961, Mandela alizindua jeshi lake la Umkhonto we
Sizwe kupigana dhidi ya utawala wa wazungu.
No comments:
Post a Comment