Mwanza.Raia
wa China ambaye ni meneja uzalishaji katika kampuni ya ujenzi Shen
Hai,46, amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuchana noti ya shilingi 10,000
ambayo ni mali ya Serikali ya Tanzania.
Akisomewa
mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mkoa Janeth Masesa, Mwendesha
Mashtaka wa Serikali, Castus Ndamugobas alidai kuwa Mchina huyo
alitenda kosa hilo mnamo Desemba 3 mwaka jana katika maeneo ya uwanja wa ndege
Wilaya ya Ilemela majira ya saa 10:30 jioni ambapo kwa makusudi aliichana noti
hiyo yenye namba AY3748043, ambayo thamani yake ni Sh10,000 mali ya
Serikali ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment