Mwalimu wa madrasa ya Ali Munawar,
ustaadhi Mohamed Ngulanjwa (36) wa Mbagala Mianzini jijini Dar es Salaam,
ameuawa baada ya kumchinja mwanafunzi wake.
Ustaadhi huyo aliyekuwa mwalimu wa madrasa na shule ya awali ya Ali Munawar, alimchinja mwanafunzi huyo
ijumaa saa 12.10 jioni kwenye eneo la madrasa baada ya kutenganisha kichwa na
kiwiliwili
(hudugu)
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Temeke, Jonathan Shana, akizungumzia mauaji hayo, alisema tukio hilo la
kinyama, lilishuhudiwa na wananchi waliomuua ustadhi huyo.
Alisema baada ya mwalimu kumuua
mwanafunzi wake wa kiume alichukua kisu alichotumia pamoja na msahafu na
kukimbia.
"Ilidaiwa kuwa alimchukua mtoto
huyo , kumlaza chini kisha kumchinja kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili na
kutelekeza vipande vya mwili wake kwenye varanda," alisema Kamanda Shana.
Baada ya mauaji hayo mtuhumiwa
alianza kukimbia lakini wananchi walimvamia na kumshambulia kwa mawe na kila
silaha iliyokuwa karibu na kumuua papo hapo.
Shana alieleza kuwa polisi walifika
eneo la tukio na kuchukua maiti hizo na kuzipeleka hospitali ya Temeke.
Hata hivyo alisema jina la mtoto huyo
mwenye umri kati ya miaka 10- 12 halikufahamika na polisi inaendelea na
uchunguzi
No comments:
Post a Comment