Visitors


hit counter

Breaking News

728-banner


web counter

OnAir

Saturday, 25 January 2014

MAGAZETI YA UDAKU BWANA NOMA! ET DIAMOND KAWA BEKI TATU KWA WEMA SEPETU???? JIONEE HAPA

NYOTA asiye na mpinzani katika muziki wa kizazi kipya kwa sasa, Nasib Abdul ‘Diamond’ ambaye amerejesha penzi lake kwa malikia wa filamu Tanzania, Wema Sepetu, anadaiwa kuhamia nyumbani kwa mrembo huyo mwenye kuongoza kwa mikasa Bongo, aishiye Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

" LINAPATIKANA MTAANI LEO HADI jumapili DAKA KOPI YAKO"

Read more ...

Sunday, 19 January 2014

HATIMAYE MASOGANGE AMTAJA ALIYE MTUMA MZIGO WA DAWA ZA KULEVYA

HATIMAYE yule Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ aliyepatikana na hatia ya kuingiza nchini Afrika Kusini malighafi haramu aina ya ephedrine, amemtaja mtu aliyemtuma mzigo huo kuwa ni Mkongomani, Risasi Jumamosi limedondokewa na ‘kismati’.
Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’.
 Katika mahojiano ‘spesho’ na gazeti hili yaliyofanyika kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga, Mwenge, Dar es Salaam, juzi, Masogange aliamua kumwanika kigogo huyo huku akimtaja jina bila kuuma maneno.
Melisa Edward
 TWENDE PAMOJA
Risasi: Masogange tumekuita leo hapa kwa ajili ya mahojiano maalum. Tangu umerudi Bongo toka Afrika Kusini ulikokutwa na ule msala wako, naamini hujawahi kuzungumza na chombo chochote cha habari. Uongo, kweli?
Masogange: Kweli kabisa.
Risasi: Risasi linakukaribisha tuzungumze mambo muhimu, lakini kubwa kuliko yote, hebu mtaje mtu aliyekutuma kubeba ule unga ambao ulikamatwa nao Afrika Kusini.
Masogange: (akionesha sura ya umakini) kusema ule ukweli, ni…(anamtaja jina). Huyu bwana ndiye aliyeniponza kwa yote yale.
Risasi: (bila mshtuko baada ya kutajwa kwa jina hilo). Huyo mtu ni Mtanzania kweli?
Masogange: Hapana, ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ila anaishi Tanzania miaka nenda, miaka rudi.
Risasi: Sasa Masogange, huyu mtu ilikuwajekuwaje hadi akakutuma kupeleka mzigo ule Afrika Kusini, hapo pana utata kidogo.
Masogange: Wengi hawajui. Iko hivi, siku ile (Julai 5, 2013) mimi nilikuwa nasafiri kwenda Sauz kwa mambo yangu tu. Nilipofika pale Uwanja wa Ndege (Julius Nyerere International Airpot) nilimkuta huyo mtu.
Risasi: Naye akiwa anasafiri kwenda huko?
Masogange: Hapana. Yeye tunafahamiana kwa muda mrefu, aliponiona aliniuliza kama nakwenda Sauz, nikamwambia ndiyo. Akasema anaomba nimbebee mizigo yake ya sukari.
Nilimkatalia, lakini akasema kuna mtu atanipokea Uwanja wa Ndege (wa Kimataifa wa Oliver Tambo) uliopo (Kempton Park) Johannesburg.
Basi nilimkubalia, lakini…
Risasi: Subiri kwanza Masogange.  Hapo una maana wewe kazi yako ilikuwa kubeba tu, baada ya kutua kule ungekutana na mwenye mzigo, Je, uliuangalia mzigo wenyewe kama kweli ni sukari?
Masogange: Ndiyo. Nilimwambia anifungulie nione kama kweli ni sukari, akafungua begi moja, nikachungulia na kuona kweli ni sukari nyeupe!
Nilimwambia kama anataka nimsaidie kuufikisha Afrika Kusini, apeleke mpaka kwenye ndege ili kunipunguzia kazi ya kubebabeba. Nikifika Sauz nitamtolea huyo mtu sukari yake.
Basi, akapeleka mpaka kwenye ndege, mimi nikapanda na safari ikaanza.
Risasi: Subiri kidogo Masogange. Wewe ulikamatwa na mtu anayedaiwa ni ndugu yako, Melisa Edward. Mbona humtaji?
Masogange: Oke, yule tulikuwa safari moja tu. Lakini yule Mkongomani anajuana na mimi.
Risasi: Oke, endelea.
Masogange: Tulifika uwanja wa ndege salama. Nikashuka na yale mabegi nayo, lakini cha ajabu wakatokea askari na kutukamata.
Waliniuliza nimebeba nini? Nikawaambia sukari, wakasema siyo sukari, wakanitaka nilambe. Kulamba hivi, ndiyo nikajua kweli siyo sukari, tukawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kwenye vyombo vyao vya sheria kwa hatua zaidi.
Risasi: Pole sana. Kwa hiyo yule mtu ambaye angepokea mzigo kule Sauz ulimwona ulipotua uwanjwa wa ndege?
Masogange: Sikuwa namjua kwa sura, nilipewa mawasiliano yake tu. Kuna uwezekano alituona wakati tumekamatwa na polisi maana tulizungukwa na watu wengi.
Risasi: Unakumbuka yalikuwa mabegi mangapi ya hiyo ‘sukari’?
Masogange: Hata sikumbuki vizuri mimi, nilishachanganyikiwaga jamani, yalipita yale.

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari kwa kuwaonyesha picha ya Agnes Gerald ‘Masogange’ katika simu ya samsung Tab.

ANAYEMJUA MWAKYEMBE
Siku chache baada ya mlimbwende huyo kunaswa Sauz, Bongo, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe alimtaja kijana ajulikanaye kwa jina moja la Mangunga kwamba ndiye aliyedaiwa kuwa na video queen huyo ndani ya ndege kwenda Afrika Kusini.
Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao baada ya kukamatwa kuwa ni Agnes Jerald ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989.
Mwakyembe aliamuru kijana huyo asakwe na kukamatwa ili kujibu mashitaka ya kusafirisha madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine kwa Tanzania huku Sauz ikisema ‘unga’ huo ni ephedrine ambao si wa kulevywa bali ni malighafi haramu.
Nassoro
 Masogange na mwezake, Melisa walikamatwa Julai 5, mwaka jana kwenye uwanja huo wa ndege nchini humo wakiwa na madawa hayo yaliyokadiriwa kuwa na  thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Kesi yake iliendeshwa na Mahakama Kuu ya Gauteng iliyopo Kempton Park nchini humo na alikutwa na hatia ambapo alihukumiwa kwenda jela miezi 32 au kulipa faini ya randi 30,000 (shilingi milioni 4.8). Masogange alilipa faini huku mwenzake, Melisa akiachiwa huru kukutwa hana hatia.

Source: GPL
Read more ...

HAPPY BIRTHDAY KWA BLOGGER HUSSEIN WA UJANA TZ, MDAU MKUBWA WA BONGOCLAN TANZANIA


Read more ...

HATIMAYE YULE MBONGO ALIYEKAMATWA MAREKANI KWA KOSA LA KUBAKA BIBI WA MIAKA 62 AACHIWA HURU, SOMA MKASA MZIMA HAPA

Steve Konyagi.
Mwaka 2010 kwenye mwezi wa 11 Steve Konyagi Mtanzania anayeishi mji wa Lynn Massachesetts nchini Marekani alishitakiwa na Mtanzania mwenzake (jina kapuni) kwamba amembaka demu wake Mmarekani wakati hua aalikua na miaka 62 na kufikishwa mahakami na kuwa nje kwa dhamana.
Steve Konyagi alikuja Marekani mwezi wa 8 mwaka huo 2010 kabla hata hajakaa sawa akakutana na balaa hilo la kubaka ambalo kama utapatikana na kosa kifungo chake ni miaka 20 mpaka 40. Steve Konyagi Tanzania anatokea maeneo ya Sinza.
wakati Steve Konyagi alipokua akiendelea na kesi yake ya kubaka bibi Mmarekani wa miaka 62 aliibuka dada mwingine Mtanzania (jina kapuni) aliyewahiishi DMV miaka ya nyuma na kudai nae kabakwa na Steve Konyagi hiyo ilikuwa mwaka 2011. Mahakama iliamua kuondoa dhamana kwa Steve Konyagi na kuMsweka ndani kuanzia wakati huo huku ikiendelea kusikiliza kesi hiyo iliyochukua takriban miaka mitatu.

Vijimambo baada ya kupata tetesi za Steve Konyagi kuwa huru ilinyanyua simu na kumtwangia na yeye bila ajizi alinyanyua na kuanza kuelezea kisa kizima. Vijimambo ilitakakufahamu kulikoni na Steve Konyagi akaanza kwa kusema mwaka 2010 kwenye mwezi 8 aliwasili Marekani baada ya kushinda Creen Card na alifikia kwa dada mmoja anayeitwa Adela ambaye yupo Massachusetts miaka mingi.
Jumamosi moja ya mwezi wa 11, 2010 huyo Mtanzania aliyemshitaki walifika nyumbani kwao akiambatana na demu wake huyo Bibi Mmarekani wa miaka 62 wakati huo sasa hivi huyo bibi atakua na miaka 65. Mara baada ya kufika nyumbani kwao kama ilivyoada ya Steve Konyagi ni mtu wa mchupa sana na baada ya kutembelewa na wageni walianza siku yao kwa kupiga mitungi mpaka usiku mnene na demu wa mshikaji akawa amepagawa na Steve Konyagi mdada akimtia majaribuni mshikaji wake. Baada ya mitungi kukolea Demu wa mshikaji alishindwa kuvumilia alimtonya Steve kwamba kwake yeye hajiwezi na Steve tangia aje Marekani alikua hajaona ndani alikua na kinenge kikali pamoja na hivyo bado alishindwa kula uroda kwa demu wa mshikaji lakini kilichotokea demu kulazimisha sana alichoambulia ni kula pipi kijiti.
 wakati huo mshikaji alikua amezidiwa kwa mchupa alipozinduka alihisi swaiba wake amemtenda kitu mbaya na alipoanza kudodosa demu alijitetea kwa kumsinginzia Steve kwamba amembaka ndipo mshikaji pamoja na kwamba yule demu alikuwa mkubwa kiumri jamaa hakukubali alionelea yaishie mahakamani.
Read more ...

DIAMOND KATISHA, ONA GARI LAKE JIPYA NA SWAGA AKIWA NALO MAENEO, INAUZWA ZAIDI YA MILIONI 100

Diamond Platnumz new Car 2014

Hahaaaa kweli diamond noma sana, wanaosema ana hela kibao hawajakosea kabisa kwani kwa mafanikio aliyonayo na anaendelea kupata sidhani kama atafilisika leo. Najua kuna wengi mnaweza bisha na kusema kwani Mr Nice alikua wapi na leo yupo wapi, but ukweli ni kwamba Diamond na Mr Nice wanautofauti mkubwa katika kupanga na matumizi ya mshiko.

Hii si siri tena kua kwa sasa Diamond ndo anaongoza kwa kua msanii anaelipwa mshiko mrefu kuliko wote hapa bongo na nahisi anaelekea kua hata Afrika Mashariki. Nina ushahidi kidogo tu kua admin wenu wa Tzfix nilipokua likizo katika jiji la Mwanza Diamond alipiga show katika jengo la Buzuruga Plaza na kulipwa shilingi Milioni 23. Sidhani kama kuna msanii yoyote wa bongo alishawahi kulipwa mshiko huo kwa show moja, ili afikishe mshiko huo nahisilazma apige kuanzia show 3 hadi 4 ili amfikie Damond.

Diamond Platnumz new Car 2014

Tuache Brabra na tuende kwenye utamu wenyewe, kama mnakumbuka miezi michache iliyopita msanii Diamond alinunua gari aina ya Toyota Prado na ilikua gumzo sana mtandaoni na kwenye magazeti ya udaku. Sasa baada ya mshiko kuongezeka kaamua kununua gari ambayo ni funiko yani hakuna msanii mwenye kiburi wala jeuri ya kununua gari hiyo. Maana akijaribu tu basi ujue uchumi wake utatetereka mbaya, nayo si nyingine ni Toyota Land Cruser V8 Mpya Kabsa.


Katika fukunyuafukunyua ya timu yetu ya Tzfix tukagundua kua ili mtu aweze nunua gari hiyo ni lazima awe na dola za kimarekani 70,000 au ambayo ni zaidi ya milioni 110. Hakika ni gari ya ukweli sana na hapa bongo wanaotumia magari haya kwa wingi ni watu wenye vyeo vikubwa serikalini mfano JK, Pinda na baadhi ya mawaziri.
Diamond Platnumz new Car 2014
Timu nzima ya Tzfix inapenda kumpongeza msanii Diamond kwa mafanikio aliyofikia kwani haijawahi kutokea hapa bongo msanii yeyote kumiliki gari ya aina hiyo na ya mkwanja mrefu kiasi hicho. Itakumbukwa kua marehemu kanumba aliwahi kumiliki V8 lakini hii ya Diamond ni noma sanaaaaaaa. Kweli Mziki unalipa hasa kama wasanii wa bongo wataichukulia kama kazi.
Read more ...

Sunday, 5 January 2014

HAYA NDIO YANAFANYIKA KWENYE CLUB ZA HUKO KENYA,TAZAMA HIZI PICHA 11 WANAWAKE WALIVYOWATUPU JUKWAANI!














Read more ...

BOTI YA KILIMANJARO 2 YANUSURIKA KUZAMA NUNGWI


Newss Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka chanzo chetu cha habari kinasema boti ya MV Kilimanjaro II mali ya Bharlesa imepigwa na dhoruba maeneo ya kisiwa cha Nungwi imekosakosa kuzama ikiwa inatoka Pemba kuelekea Unguja kwa mujibu wa mtoa habari wetu ni kwamba kuna Abiria wengine wameachwa baharini pamoja na mizigo mingine kutokana na Boti hiyo kupigwa na wimbi kubwa na kuyumba na kujikuta kuwadondosha abiria pamoja na mizigo katika bahari kwa sasa boti hiyo inaendelea na safari, mabaharia wa Boti hiyo wamejitahidi,
Read more ...

RAIS KIKWETE AFUNGUA HOSPITALI YA KMKM KIBWENI, ZANZIBAR LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya KMKM Kibweni mjini Zanzibar leo. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya KMKM Kibweni
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali baada ya ufunguzi rasmi wa Hospitali

Askari wakakamavu wa kike wa KMKM wakiwa wamesimama kumlaki Rais Jakaya Mrisho Kikwete  alipowasili kwa a ufunguzi rasmi wa Hospitali ya KMKM Kibweni mjini Zanzibar leo.
Read more ...

DESIGN MPYA YA 2014 YA MIKOBA NA VIATU VILIVYOTENGENEZWA KWA KUTUMIA VITENGE


Tunapokaribisha mwaka mpya 2014 ni vyema pia kupanga mambo mengine upya na kuyaweka katika ubora ili kuweka tofauti kubwa kati ya yale tuliyoyafanya mwaka uliopita na yale tutakayoyafanya mwaka huu.

Basi katika swala la mavazi na viambatana vyake nimeona ni vyema kushare nawe viatu vya wanawake na wanaume na mabegi ya kisasa yaliyotengenezwa kwa kutumia vitenge. ni ubunifu wa hali ya juu tazama hizo picha unaweza kukubali ninachokuambia.












Read more ...

Mchina kizimbani kwa kuchana noti ya Sh10,000


Mwanza.Raia wa China ambaye ni meneja uzalishaji katika kampuni ya ujenzi  Shen Hai,46, amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuchana noti ya shilingi 10,000 ambayo ni mali ya Serikali ya Tanzania.

Akisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mkoa Janeth Masesa, Mwendesha Mashtaka wa Serikali,   Castus Ndamugobas alidai kuwa Mchina huyo alitenda kosa hilo mnamo Desemba 3 mwaka jana katika maeneo ya uwanja wa ndege Wilaya ya Ilemela majira ya saa 10:30 jioni ambapo kwa makusudi aliichana noti hiyo  yenye namba AY3748043, ambayo  thamani yake ni Sh10,000 mali ya Serikali ya Tanzania.
Read more ...

Thursday, 2 January 2014

Picha za uzinduzi wa video 'Roho Yangu' ya Rich Mavoko,Maisha Club

  
                               
  Msanii Rich Mavoko usiku wa kumkia leo alizindua rasmi video yake ya  wimbo wa 'Roho Yangu', katika ukumbi wa Maisha Club iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam,katika uzinduzi huo Rich Mavoko alisindikizwa na wasanii mbalimbali  wakiwemo Jux Vuitton,Barnaba,Dully Sykes,Shetta,Mr Blue na wengineo.

Angalia picha hapa.


Read more ...

Mwamvita Makamba atoa ushauri kwa wasichana kufuatia sakata la Jackie Cliff kukamatwa na Madawa ya Kulevya


Mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini Mzee Yusuf Makamba, Mwamvita Makamba kupitia ukurasa wake wa twitter amewashauri wasichana wa Tanzania kujiepusha na tamaa na maisha ya dezo. Mwamvita ambaye ni ‘Business Performance Partner: Corporate Affairs’ wa kampuni ya Vodacom, nchini Afrika Kusini, ametoa ushauri huo kufuatia kukamatwa kwa mrembo wa video za muziki nchini, Jackie Cliff aliyekamatwa mwezi huu nchini China na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 223.

Huu ndio ujumbe wake alioupost Desemba 26.

#1."Girls; Kama huna akili - hujasoma na huna kazi, kama ni mvivu na sio mbunifu,mpenda dezo na huwezi honest living mara mia 'buzi' sio 'sembe'," aliandika kwenye Twitter.

#2."Girls: get inspired na jasho la bidii binafsi sio maisha ya dezo.Tengeneza chako ndio upate fahari. Binti Amka –Unaweza."
Read more ...

Justin Bieber amshirikisha Lil Wayne kwenye wimbo wake mpya,'Backpack' usikilize hapa




Read more ...

Nakukaribisha ukitazame kipindi cha Wema Sepetu 'In My Shoes' sehemu ya nane ( House Renovation)


follow the you tube video below


Read more ...

HIZI NDIZO MUSIC TOURS AMBAZO DIAMOND HATOZISAHAU KWA MWAKA 2013


Ni moja ya matukio ambayo kila nikiyatazama kwenye maktaba yangu ama nikiyakumbuka najiskia ni kias gani nina deni kubwa la kutowaangusha mashabiki 
wangu, ni mapenzi ya hali ya juu,me ni nani watu waache kazi zao waandamane kunitazama nikipita mtaani??
Nawapenda sana watu wangu & always i will do the best for you’,
alisema diamond

 



 















CONGO













Read more ...
Designed By Published.. Blogger Templates