Diamond Platnumz aka Prezident wa WCB ametoa kali na mpya
kwa kuamua kujiita 'DoMo' kupitia ukurasa wake wa Instagram kama unavyo ona
hapo chini. Yawezekana amefikia hatua hiyo baada ya watu wengi kumkashifu mara
nyingi sababu ya mdomo wake.
Breaking News
728-banner
OnAir
Friday, 29 November 2013
BABA KANUMBA ATOA MASHARTI MAGUMU KWA WALE WOTE WANAOTAKA UZAO WAJITOKEZA, WATIMKA
Baba wa
marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa.
BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa amefunguka kuwa baada ya kutangaza kuwa wanawake wanaotaka uzao wake wajitokeze azae nao, wamejitokeza kumi lakini akawapa masharti, yakawashinda.
Akizungumza na mwandishi wetu, baba Kanumba aliweka bayana kuwa warembo hao waliojitokeza aliwapa sharti la kwenda kupima Ukimwi lakini ajabu wote waliingia mitini.
“Wamejitokeza vizuri lakini nashangaa wote wamekuwa wazito katika suala la kupima Ukimwi wameingia mitini, kama wapo wengine watakaolimudu sharti hilo, nawakaribisha,” alisema baba Kanumba
Labels:
Lifestyle & Fashion,
News
Picha sita za muonekano wa jengo jipya la uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) baada ya ujenzi Utakapokamilika
Hapa ni mahali ambapo abiria watakuwa wakisubiri kabla ya kwenda kupanda ndege (Departure Lounge)
Muonekano wa
ndani ya jengo
Jinsi patakavyoonekana kutokea angani
Upande wa maegesho ya ndege
Ujenzi wa jengo hilo umepangwa
kufanyika kwa awamu mbili. Kukamilika kwa awamu ya kwanza kutawezesha uwanja
huo kufikia uwezo wa abiria mil 3.5 kwa mwaka tofauti na jengo la sasa ambalo
uwezo wake ni abiria mil 1.5 kwa mwaka. Awamu ya pili itaongeza uwezo huo hadi
kufikia abiria mil 6 kwa mwaka. Baada ya kukamilika jengo hilo, jengo lililopo
sasa (Terminal II) litatumika kwa shughuli za abiria wanaosafiri ndani ya
Tanzania tu.
Labels:
Lifestyle & Fashion,
News
"Yaliyotokea kwenye Msiba wa Sharo Milionea sitakati yajirudie kwangu siku Nikifa"....Kitale
Muigizaji
na mwimbaji nchini Kitale yuko Tanga alipoenda kuhudhuria Dua ya kumuombea
marehemu Sharo Milionea ikiwa ni mwaka mmoja tangu afariki dunia kwa ajali
mbaya ya gari.
Kitale
ambaye ndiye msanii pekee aliyefika Tanga siku ya juzi amesema kuwa amejifunza
mambo mengi katika msiba wa rafiki yake Sharo Milionea, ikiwa ni pamoja na
misiba ya wasanii wengine waliotangulia mbele ya haki, Kanumba na Sajuki.
Akiongea
kwa njia ya simu na Edson Mkisi katika kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times
Fm, Kitale amesema kutokana na funzo alilopata ameampa ujumbe mama yake ili
kwamba pindi atakapotangulia mbele ya haki mambo hayo yasijirudie kwake.
“Nimejifunza
vitu vingi na nimejua marafiki walio wema na marafiki wasio wema. Ina maana
kwamba kuna marafiki wanafiki na marafiki wasio wanafiki. Amesema Kitale.
“Kuna
vitu vingi nimejifunza baada ya kuondoka marehemu Steven Kanumba, nimejifunza
baada ya kifo cha Sharo Milionea, na nimejifunza baada ya kifo cha Sajuki.
Nimejifunza vitu vingi sana sana sana.” Amesisitiza.
“Ina
maana hata mimi kama ntatangulia kuna mambo ambayo nimeshamweleza mama yangu na
nimeshaieleza familia yangu, nafikiri hakitakuja kutokea kama kilichotokea kwa
wenzangu. Nimejifunza vitu vingi hasa ukiwa msanii...” Kitale ameiambia Hatua
Tatu.
Hata
hivyo Kitale alikataa kueleza ujumbe huo na kudai kuwa ni siri kati yake na
familia yake kwa kuwa hafahamu nani atatangulia kati yake na wazazi wake.
Kitale
amewashauri wasanii kumkumbuka Mungu wakati wanapoendelea na shughuli zao na
ndio sababu watu wengi wanaamini kuwa asilimia kubwa ya wasanii ni ‘Freemason’,
na kwamba hiyo inatokana na kitendo cha wasanii hao kumsahamu Mungu wao.
(November 27,2012) ndio siku ambayo marehemu
Sharo Milionea alizikwa huko Tanga.
Labels:
Intertainment,
Lifestyle & Fashion
WATUMIA NYETI YA MWANAUME KAMA KEKI YA BIRTHDAY.......CHEKI HAPA!!
Katika hali
inayozidi kuonesha kuporomoka kwa maadili na heshima miongoni mwa wanawake,
wasanii fulani nchini Nigeria wamefanya kali ya mwaka pale walipotengeza keki ya Birthday ya rafiki yao ambayo ilipambwa na taswira ya NYETI za kiume ambapo rafiki huyo alikuwa akiilamba kila wakati kama anavyoonekana pichani hapo juu
wasanii fulani nchini Nigeria wamefanya kali ya mwaka pale walipotengeza keki ya Birthday ya rafiki yao ambayo ilipambwa na taswira ya NYETI za kiume ambapo rafiki huyo alikuwa akiilamba kila wakati kama anavyoonekana pichani hapo juu
Labels:
Lifestyle & Fashion,
Udaku
KWANINI BAADHI YA WATU WANACHUKIA MAFANIKIO YA DIAMOND? ...TATIZO NI ‘BEI YA MKAA’....SOMA ZAIDI HAPA
Wakati mwingine inahitaji roho ya paka kuendelea na nguvu
kufanya kile unachofanya wakati watu wanaendelea kukudhihaki.
Zaidi ya muziki, kuna kitu gani kizuri kinachoitangaza Tanzania nje ya nchi kwa sasa? Tusaidiane kuuchambua ukweli huu unaomezeka kwa fundo la mate la kulazimisha kinywani.
Ni lini mara ya mwisho Tanzania imefanya vizuri kimataifa kwenye soka? Hakuna habari njema zaidi ya kuendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu, iwe kwetu hata nje
Ni lini mara ya mwisho mkimbiaji riadha wa Tanzania ameshinda mbio zozote za kimataifa? Hakuna.
Kimichezo ni kama bado tumeendelea kuwa wasindikizaji tu. Au umesahau jinsi Selemani Kidunda alivyodundwa mwaka 2012 kwenye mashindano ya Olimpiki? Ukitoa mwaka 2005 pale Nancy Sumari alipokuwa Miss World Afrika, ni lini mrembo yeyote wa Tanzania amewahi kuiletea sifa nchi yetu?
Ni nini hasa kinachoweza kuifanya Tanzania kuipeperusha bendera yake kwenye jukwaa la kimataifa kwa sifa nzuri? Au labda kipindi hiki tumegeuka kuwa mabingwa wa biashara ya dawa za kulevya na Watanzania ndio wamekuwa vinara wa kukamatwa kila kukicha nchi za nje.
Angekuwepo Kanumba na zile jitihada alizokuwa akizifanya, labda tungesema Bongo Movies ilikuwa inaelekea kuwa njia nzuri ya kutupa heshima pia. Lakini tangu afariki, hakuna mwingine anayeonesha dalili za kufanya kile alichokuwa anakifanya na filamu zetu zimeendelea kuwa za nyumbani pekee.
Hivyo, ukiangalia kwa mifano hiyo, ni muziki pekee wenye matumaini ya kuliongezea ‘kiki’ jina la nchi yetu kwenye ‘google search’. Lakini kama muziki ndio unaonekana kuwa kitu muhimu kinachoitangaza Tanzania, mbona wale wanaofanya vizuri kwa kutuwakilisha nje tunawabeza?
Mpaka muda huu, ukimtoa AY, hakuna msanii mwingine wa Tanzania anayevuma kimataifa kama alivyo Diamond Platnumz. Amefanikiwa kiasi cha hivi karibuni kumshirikisha staa wa Nigeria Davido kwenye remix ya wimbo wake, Number 1 na video iliyogharimu si chini ya dola 25,000 iko mbioni kutoka. Amekuwa ni msanii mwenye kujituma, kutake risk na kutochoka kujaribu kufanya kile wengi wamekuwa wakikiogopa kufanya. Lakini bado kuna watu wengi hawaoni anachokifanya na wameendelea kumkejeli.
Wanasema hakuna binadamu aliye mkamilifu, lakini pamoja na kwamba unaweza kumnyonga mnyonge, ni vyema kukumbuka kumpa haki yake. Ni asili ya mwanadamu kuumizwa na mafanikio ya mtu mwingine, na ndio kinachotokea kwa Diamond. Ameendelea kufanikiwa kiasi mpaka anaanza kuwakera wengine. Si kosa kuchukia maisha na scandal zake, lakini si kosa pia kusifia kile anachoifanyia Tanzania.

TID KUFANYA COLLABO NA MWANADADA MREMBO NA MWENYE KUVUTIA" AZEB WENDWOSEN" KUTOKA ETHIOPIA
Khalid
Mohamed aka TID (Top in Dar) ametangaza kufanya collabo na msanii mrembo wa
Ethiopia aitwaye Azeb Wendwosen.“She is called Azeb an Ethiopian Artist who is
duin a single with me currently…” TID mnyama ameandika kupitia Instagram na
kuweka picha ya msanii huyo mrembo kwelikweli.
Baada ya kumtafuta kwa simu
kuzungumiza swala hilo big boss huyo wa Top Band amesema atatoa taarifa kamili
juu ya collabo hiyo soon.
Tazama picha zake hapa
Labels:
Intertainment,
Lifestyle & Fashion
TAMBUA MADHARA YA KUTOSHIRIKI TENDO LA NDOA KWA MUDA MREFU...(18+)
Aise, kwa kawaida kama wewe si
mgonjwa wa aina yoyote ile, kwa maana ya ugonjwa ku-offset system ya mwili,
madhara ya kutofanya tendo la ndoa kwa muda mrefu ni makubwa kuliko
unavyofikiria as long as upo ktk active range of age! madhara
yapo ya Negative na positive.
Mfumo wa fahamu (central novous system) hutumia zaidi tendo la ndoa ku-radiate energy inayowezesha ubongo pamoja na mifumo mingine ya mwili kufanya kazi zake vizuri bila msongo. Suala hapa si lazima uke na uume kukutana na kuingiliana (penetration) ila tu stimulation(msisimko) inayofikisha mtu
kileleni (orgasms). kwahiyo, nature(asili) inataka mke na mme kufanikisha zoezi hili maana ni jambo muhimu kama ilivyo kutoka jasho mwilini maana sio tu mwili unaondoa uchafu ndani lakini pia inacontrol joto la mwili (cooling effect).
Anayesema amekaa zaidi ya mwaka na hana madhara.., well sikatai wala sikubali maana hatuna ushahidi nalo lakini zipo njia nyingi mbadala kama kutumia sex toys,

dildo(vibrant artificial penis zitumiazo umeme), usagaji n.k. sasa sijui
yeye anatumia ipi sababu vichocheo anavyo mwilini and, it's brain iniciated.
Ukidumu bila tendo la ndoa muda mrefu, baadhi ya madhara madogomadogo nikama haya:
Hasira za mara kwa mara ktk mambo madogo,
kupendelea sana kuangalia picha za uchi,
Kusahausahau,
Kupendelea story za mapenzi,
Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mke),
Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu),
Kuumwa na kichwa,
Kukakamaa mgongo (wanaume),
Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba,
Kupoteza umakini ktk kazi (efficiency),
Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno,
Waweza ku-develop tabia mpya ambayo hukuwahi kuwa nayo ili iwe mbadala kama ulevi…

MAMBO YAMEANZA!! ZITTO KABWE AANZA KUMSHUGHULIKIA MMOJA BAADA YA MWINGINE, AMPANDISHA POLISI HENRY KILEWO
WAKATI Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma zinazomkabili, yeye
ameamua kukimbilia polisi akimshitaki mmoja wa viongozi wenzake.
Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.
Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto.
“Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine,” alisema Kileo.
Zitto kutwa nzima ya jana hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kufafanua mashitaka aliyofungua polisi. Simu zake zote za kiganjani zilikuwa zimezimwa.
-Tanzania daima.
MAAJABU…NYOKA WAMFANYIA MTU MASAJI KWA GHARAMA YA $47...! CHEKI PICHA ZA TUKIO HAPA
UNAPENDA kufanyiwa masaji na nyoka? Unaweza kukaza
roho na usiogope kung’atwa? Kama ndio basi nenda nchini Indonesia utaipata kwa
raha zako.
Masaji hiyo inapatikana Bali Heritage Reflexology and Spa
huko Jakarta, Indonesia ambako wanaweza kukuondolea uchovu wako wa siku
nzima kwa massage ya nguvu inayofanywa na nyoka mkubwa.
Masaji hiyo inafanyika kwa nyoka huyo kuwekwa juu ya
mwili wa mteja na mengine huachiwa yeye nyoka afanya yake. Ili kupata huduma
hii mteja hutakiwa kulipa dola 47 ambazo ni zaidi ya shilingi 76,000 za
Tanzania.
Labels:
Lifestyle & Fashion,
News
Maiti hufukuliwa makaburini ili kubadilishwa nguo huko Indonesia
Pichani ni baadhi ya wafu
waliofukuliwa kaburini na kuvishwa nguo Indonesia.
KILA mwaka huko Tana Toraja,
Indonesia, wafu (au maiti) hufukuliwa kutoka makaburini ili kubadilishwa nguo.
Watu wa eneo hilo wa kabila la Toraja wana mila za ajabu kuhusu vifo na
maisha yanayofuata
baada ya mtu kufa.
Wao mtu akifa hutakiwa kuzikwa katika
eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia.
Idadi kubwa ya watu wa eneo hilo ni
Wakristo, wanaofuata ni Waislam na wengine ni Wapagani ambao
wanajulikana kwa imani au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya
Mababu”.
Torajan huishi katika maeneo ya
milimani na hawataki kujulikana sana katika jamii, japokuwa wana mila na
desturi zao zilizoenea katika jimbo la Sulawesi.
KIBURI YAPESA::PREZZO AONYESHA BUNDUKI YAKE YA "AK 47" IKIWA NI YA DHAHABU TUPU.!!
Prezzo amekuwa akizungumza na haters wake kwa vitendo, kwa kupost Instagram picha mbalimbali zinazoonesha kuwa hana ‘njaa’ kama walivyowahi kusema baadhi ya ‘maadui’ zake wakiwemo Huddah pamoja na dada mwingine aitwaye Ashley Toto waliowahi kusema amepigika
.
Katika picha ya bunduki Prezzo aliandika “Nobody lied…….. iam a star & got a chopper in the car #TrulyUnruly #Rapcellency”
Katika picha nyingine shemeji yetu Prezzo ameonesha saa yake ya Rolex pamoja na pete vyote vikiwa ni Gold.
“I know u
want the finer things in life & I can get em 4 u, all u have to do is
decide how bad u want em’ #Rolex KissThePinkyRing #Rapcellency #TrulyUnruly”
aliandika Prezzo katika picha hii
Labels:
Intertainment,
Lifestyle & Fashion
APIGIWA SIMU NA SMS ZAIDI YA MARA 40 KUTOKA KWA SHETANI
Mama mmoja toka Colorado nchini
Marekani alipokea simu ya ajabu usiku mmoja wa manane kutoka kwenye namba
1-666-666-666 na ndani ya masaa machache alipokea meseji nyingi sana kutoka
namba tofuti tofauti na zote zikiwa zimeandika ‘Satan’ kwa maana ya 'Shetani'.
Mwanamke huyo, Jenn Vest kipindi
kipindi anatumiwa meseji hizo alikuwa anasinzia wakati akiwa bado anaendelea
kumnyonyesha mtoto wake na ndipo aliposikia simu inaita ikipigwa kutoka namba
1-666-666-666.
LIJUE GARI JIPYA KABISA LINALOJIENDESHA LENYEWE:
Taarifa
ikufikie kutoka Samukawa, Kanagawa Japan ambako stori kwenye headlines ni
kampuni ya Nissan kupata furaha kubwa baada ya kufanikiwa kwa jaribio la gariwalilolitengeneza ambalo linajiendesha lenyewe. Unaambiwa
limetembea umbali wa kilometa 2.3 likijaribiwa kwenye mikikimikiki ya aina
mbalimbali barabarani kama vile kuovertake, kufata alama za barabarani, taa za
kuongozea magari na hata sehemu za watu kuvuka barabara.
Nissan wamesema wanalengo la kuanza
kuliuza hili gari miaka saba kutoka sasa, hiyo itakua mwaka 2020 ambapo gari
hili lina kamera maalum pamoja na sensors zinazofanikisha kulipa taarifa
ya tukio husika kwa wakati huo ndio maana linaweza kufanya kama inavyotakiwa
mfano kushika breki, kukanyaga mafuta na vitu vingine.
Kingine cha kushangaza, kwa mfano kwenye miji mikubwa ambayo parking ni tatizo unaweza kuliacha likajiendesha lenyewe kwenda kutafuta parking wakati wewe unawahi mahali alafu ukimaliza shughuli zako unalikuta linakusubiri likiwa limepaki vizuri kabisa.Baada ya kutazama hizo picha hapo juu, unaweza kutazama hii video kujiridhisha kikamilifu aisee japo hii video sio ya majaribio yaliyofanyika saa kadhaa zilizopita..

DIAMOND BAADA YA KUTANGAZA AJIRA SASA ATANGAZA DEMU ANAYEMPENDA JE WAMJUA
UKIFIKA katika
mtaa anaoishi mwanamuziki Diamond maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam
utaanza kuhisi kuwa kuna staa anayeishi maeneo hayo, macho ya wengi huanza
kumtazama mtu anayeelekea katika geti la nyumba anayoishi msanii huyo. (HM)
Muda wote
geti hilo limefungwa. Ili uweze kuingia ndani itakulazimu ubonyeze kengele
itakayoashiria kuwa kuna mgeni nje anahitaji kuingia ndani. Hata hivyo hauwezi
kupenya kirahisi ndani hadi uulizwe shida yako na kama hauna miadi na mtu
yeyote anayeishi ndani ya nyumba hiyo haitakuwa rahisi kuingia.
na kushuhudia ukimya wa hali ya juu ilhali kuna watu
ndani. Baada ya kufunguliwa geti tuliingia ndani na kupokewa na Diamond
aliyekuwa ameketi katika sebule iliyonakshiwa na mapambo makini ukutani huku
ikiwa na samani chache lakini za gharama kubwa.
Tulitumia saa mbili mfululizo katika mahojiano na Diamond
ambaye alifunguka kwa kila swali aliloulizwa na kujibu kwa ufasaha na ufafanuzi
mpana.
Mwanaspoti: Utendaji
kazi wako ukoje katika muziki?
Diamond: Nina mipango makini katika kazi
zangu. Mambo yote lazima yapitie kwa meneja wangu ndipo yanifikie mimi, mara
nyingi mtu hawezi kuzungumza na mimi moja kwa moja lazima apite huko na hiyo
ndiyo staili ya Diamond. Nimejipanga kuhakikisha nafanya kazi gani, kwa wakati gani
na sikurupuki tu, japo katika utengenezaji wa nyimbo zangu naweza nikapata wazo
basi hapo hapo nikatengeneza mistari.
Mwanaspoti: Utendaji kazi wako ukoje kuanzia
asubuhi hadi jioni?
Diamond: Saa tano asubuhi, nikishaamka
kitu cha kwanza ni kwenda 'gym', mara nyingi ni hapa nyumbani kama unavyoona
hapo nje kuna sehemu ya mazoezi na sehemu
nyingine
zilizopo ndani, mara nyingi hutumia muda wa saa moja. Ifikapo saa sita na nusu
huwa naanza kufanya kazi zangu lakini itategemea na ratiba zangu za siku ambazo
ndio mwongozo wangu wa kuimaliza siku. Baada ya hapo napumzika kwa muda fulani
na baadaye jioni huendelea na kazi na mara nyingi kazi zangu huwa nazimaliza
usiku wa manane.
Mwanaspoti: Unalala
saa ngapi? Na unalala kwa muda gani?
Diamond: Muda
wangu wa kulala mara nyingi ni saa kumi na moja alfajiri na kama sikuwa na kazi
nyingi studio basi nitalala saa nane usiku. Muda wangu wa kulala ni saa sita
mpaka nane kwa siku. Ila hata kama nikilala mapema kuamka ni saa tano asubuhi
ila itategemea na nini ninakifanya siku inayofuata na kama nina kazi maalumu na
ya mapema itanilazimu niamke mapema ili kuzikamilisha.
Mwanaspoti: Shughuli
gani zinazokuchelewesha mara kwa mara kulala?
Diamond: Ni kurekodi na wakati mwingine
shoo. Kwa wiki ninafanya shoo nyingi, kama ni tatu basi siku zote tatu nitalala
alfajiri. Siku nyingine zinazosalia ninalala usiku wa manane kwa kuwa huwa
nakuwa studio na sehemu nyingine ambazo hunilazimu kufanya kazi kwa kipindi
kirefu usiku.
Mwanaspoti: Kati ya usiku na mchana ni muda
upi unaopenda kurekodi?
Diamond: Kazi zangu narekodi usiku na
ndiyo muda ninaopendelea zaidi. Mara nyingi napenda kurekodi saa 7 usiku ili
niwe na muda na saa nyingine ni kuepuka lawama kurekodi mchana, kwasababu
vijana wengi chipukizi wataona napendelewa. Unajua ninapoingia studio napenda
kufanya kazi kwa muda mrefu, hata hivyo iliyo bora sifanyi bora liende na
siwezi kufanya kazi na prodyuza anayenipeleka tu, ni lazima na mimi nipime kama
kazi niliyoifanya inakwenda vile ninavyotaka au kama yeye anavyotaka ilimradi
tufanye kazi nzuri na iliyo bora.
Mwanaspoti: Unatumia muda gani kurekodi
singo moja na kwa upande wa video ni siku ngapi?
Diamond: Inategemea, inaweza kuwa siku
mbili au miezi sita lakini nyimbo nyingi zinatumia muda mwingi kwasababu wakati
mwingine naanza halafu napata shoo hivyo inanibidi nipange muda mwingine wa
kurekodi. Kuna nyimbo zangu ambazo nilizifanya kwa muda mrefu sana hizo huwa
sizisahau ikiwemo Ukimwona, Mbagala, Nataka Kulewa na nyinginezo. Nakumbuka
katika kazi nilizofanya kwa muda mfupi ni My Number One nilioufanya kwa
prodyuza Sheddy Clever kwa kipindi kifupi sana pamoja na Mapenzi Basi sambamba
na Binadamu hizi ni baadhi ya kazi ambazo hazikunipasua sana kichwa
kuzikamilisha.
Mwanaspoti: Una
prodyuza wako maalumu au studio yako mwenyewe?
Diamond: Sina prodyuza maalumu kila kazi
nitakayotaka kuifanya ninatafuta prodyuza yule ninayemtaka hata kama sijawahi
kufanya naye kazi. Ninafanya hivi nikiwa na malengo maalumu kwa kujiweka vizuri
mimi kama msanii na hata kuwapa nafasi maprodyuza mbalimbali kutia mkono kwenye
kazi ya mikono yangu. Ninaogopa kuwa na prodyuza maalumu kwa kuwa najua
atanisumbua ikiwa atajua kwamba namtegemea yeye pekee katika kazi zangu. Studio
sina kwa sasa ila nina mikakati ya kuwa na studio kwani nimeshanunua baadhi ya
vifaa.
Mwanaspoti: Unadhani ndiyo sababu
iliyokufanya ukagombana na Bob Junior au Manecky?
Diamond: Hapana haya mambo yalishapita
lakini nilijifunza mengi ndiyo maana niliamua kuja na staili hii. Naogopa
kubaki kuwa msanii ninayetegemea prodyuza fulani, bila yeye siwezi kufanya muziki,
lakini mimi ni Diamond ninaweza kufanya muziki na prodyuza yeyote naye
akaonyesha ufundi wake kupitia kazi yangu.
Mwanaspoti: Shoo gani kubwa kuliko zote
uliyowahi kufanya ambayo haijawahi kujirudia?
Diamond: Diamond Forever. Hii ilikuwa
kubwa sana ambayo sitakaa nikaisahau, ilihudhuriwa na watu wakubwa na maarufu
hapa nchini hata hivyo ilikuwa ya kipekee ambayo haijafanana na yoyote ile. Ya
pili ni ile ya Dar Live ambayo nilifanya baada ya kushuka katika helikopta ile
pia ilikuwa kubwa. Lakini kwa nje ya nchi ni Mombasa na Comoro huko nilifanya
shoo kubwa sana ambazo siwezi kuzisahau.
Mwanaspoti: Ni shoo ipi iliyowahi
kukuingizia pesa kubwa kuliko zote?
Diamond: Shoo ile ya Mlimani City ya
Diamond Forever, ile iliniingizia pesa kubwa sana na tangu pale ndipo
nilipoanza kufurahia matunda ya kazi yangu. Nilifanya shoo pia Burundi, Mombasa
na Congo shoo hizi ziliniingizia kiasi kikubwa sana cha pesa siwezi kutaja ni
shilingi ngapi lakini ni pesa nyingi ambazo sitakaa nizisahau.
Mwanaspoti: Shoo ipi ilikuwa ya bei chee
ambayo huwezi kuisahau
Diamond: Kwa kweli siwezi kusahau
nilipofanya shoo yangu ya kwanza kubwa mwaka 2009 kwenye Fiesta iliyofanyika
Dar es Salaam, ilikuwa ndiyo shoo yangu ya kwanza na kubwa wakati huo nilikuwa
natamba na wimbo Kamwambie, ilinichukua muda mrefu sana kujiandaa mimi pamoja
na madansa wangu wanne tulilipwa Sh 50,000 lakini sikukata tamaa kwani ilikuwa
ndiyo mwanzo wangu wa kujuana na watu wengi na wadau wakubwa wa muziki hapa
nchini ambao nilikutana nao kwenye ile shoo.
Mwanaspoti: Kwa hivi sasa ni shoo gani
ambayo unaweza kusema kwamba utafanya kwa bei ya chini na ni shilingi ngapi?
Diamond: Shoo ninayoweza kufanya kwa bei
ya chini kabisa ni Sh 10 milioni za Kitanzania na hii labda nione anayeniomba
nifanye shoo hiyo hayuko vizuri na pengine ni rafiki yangu na hawezi
kuninyonya, si hivyo tu itategemea pia ni kampuni gani na ni watu wa aina gani
ambao watanitaka nifanye nao kazi.
Mwanaspoti: Kwa kawaida Diamond ni msanii wa
gharama gani kwa shoo moja ndani na nje ya nchi?
Diamond: Kwa kawaida shoo moja ninafanya
kuanzia Sh15 milioni mpaka Sh20 milioni kulingana na muda nitakaofanya shoo.
Pia zile za nje ninafanya kwa gharama ya Dola 20,000 mpaka 30,000 yaani ni Sh32
milioni mpaka 48 milioni hivi kwa fedha za Tanzania na nikiwa huko nahakikisha
ninafanya kazi vile inavyotakiwa. Lakini hali ni tofauti inavyokuja shoo ile ya
uwanjani yaani hapa nazungumzia shoo kubwa zinazofanyika nje ya ukumbi, hizi
natoza Dola 20,000 ambayo ni sawa na Sh32 milioni 32 kwa fedha ya Kitanzania.
Mwanaspoti: Kuhusu madansa wako
unawachukuliaje?
Diamond: Ni kama kaka zangu na
ninawapenda sana kwani tumetoka nao mbali na wanajua kuwa tunafanya kazi pamoja
kutengeneza maisha hivyo ni kama ndugu zangu na tunasaidiana kwenye kila jambo
ukizingatia kuwa kile tunachokipata tunagawana. Kwa kweli najitahidi sana
kuwaambia hasa kuhusiana na masuala ya kimaisha, nahusika katika maisha yao ya
kila siku na nijuavyo mimi nikikosea tu mmoja akapotea kundi langu litakuwa
limeharibikiwa maana kila mtu namtegemea kwa upande wake. Kwa sasa wamejenga
nyumba zao na wanaendelea vizuri kimaisha hilo ndilo sharti langu lazima
wafanye mambo ya maendeleo kwa kile tunachokipata.
Mwanaspoti: Umesafiri nao nchi ngapi, na
kwanini unapenda kuambatana nao?
Diamond: Nimesafiri nao sehemu mbalimbali
kama Burundi, Comorro na sehemu nyinginezo ambako nimekwenda kufanya shoo, sina
tabia ya kusafiri peke yangu hata nikienda Ulaya na hata Marekani lazima niwe
nao. Ninapenda kuwa nao kwani ni sehemu ya muziki wangu na imefika wakati
nimekuwa nataka mapromota kuhakikisha wanatulipia mimi na madansa wangu kwa
ajili ya shoo hasa tutakapojua kuwa shoo fulani itaingiza watu wengi au
udhamini mkubwa.
Mwanaspoti: Kuna
safari ambayo umewahi kusafiri peke yako?
Diamond: Ziko nyingi, nilienda mwenyewe
kutokana na ukubwa wa shoo, lakini ni miaka kadhaa nyuma, baadaye nilijiwekea
mikakati kwamba siwezi kusafiri mwenyewe wakati shoo nahitaji kufanya na
madansa wangu, awali mapromota walikuwa wagumu kunielewa na wapo waliokataa.
Niliachana nao na kuwataka wakishajipanga na kuhakikisha kwamba wanaweza
kunichukua mimi na madansa wangu watafanya hivyo.
Mwanaspoti: Umewahi kuwatema madansa?
Diamond: Sijawahi kubadilisha madansa kwa
sababu wanajua kazi yao. Ingawa nilikuwa na madansa sita nilipokuwa naanza
muziki lakini niliachana na wawili kutokana na utendaji wao wa kazi. Wawili
hawa hawakuwa wabunifu kila siku walikuwa na staili ileile, niliamua kuchagua
vichwa ambavyo vikikaa na mimi mwishowe tunatoka na kitu makini na chenye
kueleweka. Kulikuwa na tatizo pia la kukosea stepu wakati wa shoo hili lilikuwa
likinishushia sana hadhi yangu jukwaani, hapo ndipo nilipoamua kuwaondoa.
Mwanaspoti: Kwa upande wa malipo
unawalipaje?
Diamond: Ninawalipa vizuri lakini siwezi
kutaja kiwango ila ingekuwa kwangu ningetaja, hiyo ni haki yao wao wenyewe
kutamka ila mimi siwezi kutaja. Malipo ninayowalipa yapo machoni mwa watu
wanaowazunguka, dansa kujenga nyumba kumiliki baadhi ya biashara si jambo dogo,
hivyo ninawalipa vizuri. Na hata gharama za kusafiri ndani na nje ya nchi vyote
ni juu yangu, malipo tunayoyapata tunagawana.
Mwanaspoti: Unakumbana
na changamoto zipi katika kazi yako?
Diamond: Nakumbana na mengi, kwanza
unapokuwa msanii unayeongoza lazima upate vikwazo vingi. Nakumbana na watu
wengi wanaonichukia na kunitusi bila sababu za msingi, hata hivyo nasingiziwa
vitu vingi ambavyo havipo nadhani hii ni changamoto iliyotokana na kufanya vizuri
katika muziki.
Wapo ambao
wanamwona Diamond anafanya vizuri kwenye muziki badala ya kukaa na kuangalia
nimepita wapi na wapi anaanza kutoa lawama kwamba ameibiwa na mengine ambayo
kimsingi hayana maana.
Mwanaspoti: Siku za hivi karibuni kuna
maprodyuza na wasanii wasiofahamika ambao walijaribu kutengeneza kazi yako ya
My Number One na kukutusi kupitia wimbo huo na wapo waliotunga mashairi mengine
yaliyozungumzia maisha yako kabla hujawa staa, ulijisikiaje? Na unachukua hatua
gani?
Diamond: Awali niliumia sana nilipoibiwa
mashairi ya wimbo wangu wa Mbagala, iliniuma sana kwa muda wa wiki nzima
uchungu nilioupata siwezi kuuelezea. Lakini baadaye nilikomaa, huwezi amini
niliposikia zile nyimbo nilicheka sana kisha nikawadharau sana watu waliofanya
hivyo maana nipo kwenye hii tasnia siwezi kuchukia watu wasiojua walitendalo
kwani na wao wapo katika kujitafutia riziki. Lakini hata hivyo sheria ya muziki
bado haijawa makini hapa nchini
nitachukua hatua gani mwisho wa siku
nitaacha kufanya mambo yangu ya msingi na kushughulikia wezi wa kazi zangu
ambao hata hivyo hawatabanwa kwa lile walilolifanya.
Mwanaspoti: Msanii yupi hapa Tanzania
anakutisha kama hayupo vipi huko nje ya nchi?
Diamond: Kwa hapa Tanzania sijaona
mwanamuziki anayenitisha, ila siwezi kujua mashabiki wao ndio majaji, nafikiri
kila mtu anaweza kuwa na mtazamo wake. Kati ya wanamuziki ninaowahusudu mimi
kwa nje ya nchi hasa Afrika ni P Square pekee, hawa wapo katika nafasi kubwa
sana kwenye ubongo wangu na nafikiria ni lini ninaweza kuwafikia, hiyo ndiyo
ndoto yangu daima.
Mwanaspoti: Unapokuwa juu ya jukwaa
unakumbana na vishawishi vipi ukiwa kama msanii mkubwa?
Diamond: Ninapata vishawishi vingi sana
ninapokuwa jukwaani. Kwa kweli ninashawishiwa na wakinadada, mfano kuna
mwanamke mmoja ambaye alikuwa mmoja wa mapromota wa shoo nchini Uingereza
alitaka kunibusu mdomoni kwa lazima, kitendo kile kilinifedhehesha sana na nilishindwa
nifanyeje kwani nipo ugenini na jukwaani ilikuwa ngumu sana kwangu. Wakati
mwingine wanawake wanapanda jukwaani ili wacheze na wewe mwisho wa siku
wanaingiza mikono kwenye suruali yaani sipendezwi kabisa na michezo ya namna
hii.
Mwanaspoti: Umewahi kuibiwa ukiwa
jukwaani?
Diamond: Nimeshaibiwa sana hasa katika
hizi shoo ndogo ndogo mara nyingi watu wanapanda jukwaani na kuondoka na kitu
chako. Nakumbuka nimeshawahi kuibiwa saa, pete ya dhahabu na kuna mmoja alitoa
kali ya mwaka yaani yeye alinivua nguo kwa lazima.
Mwanaspoti: Inakuwaje nje ya
muziki, unakumbana na changamoto zipi?
Diamond: Kitu ambacho ni changamoto kubwa sana kwangu ni
simu yangu ya mkononi. Kila baada ya miezi sita au mitatu nalazimika kubadili
namba yangu ya simu, nasumbuliwa sana na watu ambao hata hivyo hawana la msingi
la kuniambia. Ni kweli kwamba mawasiliano ni kitu cha msingi na
ninawapenda
mashabiki wangu lakini namba yangu inasambaa kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba
nashindwa kupokea simu za maana kwa kudhani kwamba na hao nao ni wasumbufu.
Mwanaspoti: Ina maana milio yote ya simu
hapo ni watu wanakupigia?
Diamond: Yap, unavyoona inalia kila
dakika watu wanapiga hapa. Muda mwingi hii simu ninaweka 'silent' yaani haitoi
mlio wowote kwani inaita kila dakika.
Mwanaspoti: Tuzungumzie uhusiano wako. Mpenzi
wako wa kwanza unamkumbuka? na je uliwahi kumpa shilingi ngapi?
Diamond: Mpenzi wangu wa kwanza kabisa
enzi hizo ninajifunza mambo haya sikumbuki vyema jina ila alikuwa anaishi
Tandale na mimi pia nilikuwa naishi huko na mama yangu. Sikumbuki kama nimewahi
kumhonga maana enzi hizo mimi nilikuwa napewa tu na mama yangu pesa, sikuwa na
hela yoyote ya kumpa na ilikuwa ni kwa kipindi kifupi kama miezi minne hivi,
hata hivyo tulikuwa tunaibana tu kwa siri nilikuwa mdogo.
Mwanaspoti: Kwanini mliachana?
Diamond: Kwanza nilikuwa sijajua mapenzi
ni nini. Hata hivyo haikuwa rasmi na wala nilikuwa sijawa na akili ya kupenda
sana na nilikuwa na fikra kwamba ni mchezo tu hivyo tuliachana mapema kwani
hata yeye akili yake ilikuwa haijakomaa.
Mwanaspoti: Mpenzi wako uliyekuwa naye kabla
ya kuwa staa nasikia uliachana naye baada ya kutoka kimuziki kwa nini?
Diamond: Nilimpenda sana lakini aliniacha
kabla ya kutoka. Mpenzi wangu wa kwanza alikuwa anaitwa Sarah Sadick, sijawahi
kumuhonga na ndiye mwanamke niliyewahi kumpenda sana. Wakati huo Naseeb Abdul
kabla sijawa Diamond nilikuwa nahaha kuhangaika ni vipi nitatoka kimuziki.
Msichana huyu ndiye aliyenipa hasira za kufanya muziki kwa bidii zote baada ya
kunitema na kuanza kuhangaika na wengine na aliniita majina mengi yasiyo
mazuri, kisa sina fedha. Si kwamba nilimuacha bali yeye ndiye aliyeniacha kama
zali baada ya wiki kadhaa nikatoka na wimbo Kamwambie, taratibu nikaanza kuwa
staa naye akaanza kurudi ila nilishamuondoa moyoni mwangu.
Mwanaspoti: Kwa nini mliachana? Unadhani
hakukufaa tena kwa kuwa ulishakuwa staa?
Diamond: Alinisumbua sana kutokana na
ugumu wa maisha niliokua nao kwa kipindi cha nyuma hadi kufikia 2009.
Nilimpenda sana huwezi amini nilikuwa silali usingizi kwa ajili yake. Nahisi ilitokana
na mimi kukosa kazi ndiyo maana ilifikia hatua alinipotezea. Lakini baada ya
kupata na kujulikana alinifuata lakini sikutaka tena hata baada ya kuniomba
msamaha.
Mwanaspoti: Umewahi kuwa na
wanawake wangapi tangu uwe staa?
Diamond: Sikumbuki kwa kweli wapo wengi
mno, si unajua tena wapo walionitaka na kunilazimisha nifanye hivyo, lakini
idadi kamili siwezi kukumbuka na kila siku nasumbuliwa na hawa wanawake.
Mwanaspoti: Ni wapenzi wangapi
ambao umekuwa nao kipindi kirefu na kuwapenda kama wapenzi wako?
Diamond: Nimewahi kuwa na wapenzi
wanne katika kipindi chote cha ustaa wangu na sikupenda kubadili ovyo ila wengi
wao hawakuweza kutimiza haja ya moyo wangu.
Mwanaspoti: Unaweza kuwataja majina?
Diamond: Ndiyo ila wawili
wanafahamika zaidi. Wa kwanza kabisa alikuwa anaitwa Sarah na wa pili alikuwa
anaitwa Hawa yule msichana niliyeimba naye katika wimbo 'Nitarejea', huyu
alizidiwa ujanja na Wema Sepetu ambaye naye alikuja kuondoka kwangu na baadaye
nikawa na Penieli Mungilwa.
Mwanaspoti: Mwanamke yupi unahisi
ulimpenda kuliko wote?
Diamond: Mwanamke wangu wa kwanza Sarah
Sadick huyu aliniingia sana moyoni sijajua ni kwanini. Lakini nahisi huenda kwa
kuwa awali alinipenda kweli kwa kuwa wakati huo sikuwa na kitu. Hata hivyo
nahisi ilitokana na mimi kutokuwa bize na wakati huo sikufikiria lolote zaidi
ya yeye ilitokana na kutokuwa na kazi ya kufanya. Siku hizi sina mapenzi ya
kivilee, nawaza zaidi pesa na ninaihangaikia na zaidi ni muziki wangu, hili
ndilo la kwanza kabisa linalonifanya niwe bize mapenzi baadaye.
Mwanaspoti: Umeshawahi kutongozwa
na wanawake?
Diamond: Ndiyo, wengi sana tena kuna
mmoja kati ya wanawake niliowahi kuwa nao alinitongoza yeye mwenyewe ndipo
nikawa naye na nilikaa naye katika uhusiano kwa kipindi kirefu tu. Wanaweza
kumfikiria mwanamke fulani lakini huwezi amini ukweli ninao mimi mwenyewe na
katu hawawezi hata kumhisi. Ninatongozwa sana kwenye mitandao ya kijamii,
facebook, whatsapp, Instagram na kwingineko na wapo wasichana ambao wanatafuta
namba zangu za simu na kuanza kunisumbua.
Mwanaspoti: Unapata usumbufu
wowote toka kwa wanawake?
Diamond: Ndiyo, wengi sana tena kuna
mmoja kati ya wanawake niliowahi kuwa nao alinitongoza yeye mwenyewe ndipo
nikawa naye na nilikaa naye katika uhusiano kwa kipindi kirefu tu. Wanaweza
kumfikiria mwanamke fulani lakini huwezi amini ukweli ninao mimi mwenyewe na
katu hawawezi hata kumhisi. Ninatongozwa sana kwenye mitandao ya kijamii,
facebook, whatsapp, Instagram na kwingineko na wapo wasichana ambao wanatafuta
namba zangu za simu na kuanza kunisumbua.
Mwanaspoti: Ni mwanamke wa aina gani unataka
awe mkeo?
Diamond: Kwanza ninahitaji aijue kazi yangu na ajue
kwamba mimi ni mtu maarufu hivyo akubaliane na changamoto mbalimbali
atakazokumbana nazo kwa kipindi atakachokuwa ndani ya ndoa, siyo siku mbili
anafungasha virago. Pia ajue kwamba nitamsikiliza mama yangu kwanza kabla ya
yeye hilo naliweka wazi, yeye ana nafasi yake katika maisha yangu lakini mama
yangu nimempa kipaumbele, tatu awe tayari kuishi na mama yangu. Nne awe na
akili na mwenye utambuzi na atakayeniongoza katika kazi zangu, sihitaji.
Labels:
Intertainment,
Lifestyle & Fashion
MAPENZI NOMA SANA..!! KIJANA (32) ANASWA AKIWA NA BIBI (80) CHUMBANI WAKIPONDA RAHA..!!
KUNA mengi
ya kushangaza duniani lakini hili la kijana Hamad Issa (32) kunaswa faragha na
bibi kizee Adela Mkalau (80) linaongeza rekodi ya mambo yanayoshangaza, Risasi
Mchanganyiko lina kila kitu. Tukio hilo la kustaajabisha limetokea
mwishoni mwa wiki iliyopita, nyumbani kwa bibi huyo, Yombo –Buza, jijini Dar es
Salaam ambapo wajukuu wa bibi huyo ndiyo waliomnasa. Kwa
mujibu wa chanzo chetu, wajukuu wa bibi huyo walifedheheshwa na kitendo hicho
hivyo kuwawekea mtego na kuwanasa kisha kumfikisha Hamad katika Kituo cha
Polisi Chang’ombe kwa tuhuma za ubakaji.
Katika kutafuta uhakika wa madai ya wajukuu hao, polisi wa Chang’ombe waliagiza bibi yao aitwe ili athibitishe madai hayo wakati upelelezi mwingine ukiendelea.
Sosi wetu alisema kuwa bibi aliwaacha hoi polisi baada ya kufika kituoni hapo na kukataa maelezo ya wajukuu zake, huku akisisitiza hakubakwa bali walikubaliana na Hamad. Baada ya bibi huyo kuondoa utata, polisi walikubali kumuachia Hamad kisha wajukuu wakafunguliwa kesi ya kushambulia na kudhuru mwili iliyoandikishwa kituoni hapo kwa jalada namba CHA/RB/10629/2013.
Mwandishi alifunga safari hadi nyumbani kwa bibi huyo na kuzungumza naye kuhusu tukio hilo ambapo alisema: “Sijabakwa na nimekasirishwa sana kwa kitendo cha kumpiga kijana wangu. Wawe na heshima kwa babu yao. Sisi tunapendana, kwa nini wanatuingilia?”
Alisema: “Siku hiyo Hamad wangu alikuja nyumbani kwangu tangu mapema. Nikaandaa chakula cha jioni, tukala pamoja kisha tukalala. “Tukiwa usingizini, nikasikia mlango unagongwa. Kwenda kufungua, wajukuu zangu wakaingia na kuanza kumpiga Hamad na fimbo na magongo, wakisema eti amenibaka. Hamad atanibakaje? Kwani mimi ni mtoto mdogo?
“Isitoshe wanamfahamu vizuri sana Hamad. Nipo naye mwaka mmoja na nusu sasa, leo inakuwaje wanajifanya hawamjui? Siku hizi mambo yamebadilika. Mdogo anaweza kumpenda mkubwa na mkubwa akampenda mdogo. Hakuna kosa.”
Mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwa Hamad ambapo alimkuta akiwa hoi kitandani kwa majeraha ambapo alisema: “Ni kweli bibi ni mpenzi wangu... na wale wajukuu zake wananifahamu vizuri sana. Wamenipiga sana, eti nimembaka bibi yao. Siyo kweli. Sisi ni wapenzi.” Alipoulizwa anajisikiaje kuwa kwenye uhusiano na kikongwe huyo, alijibu: “Hata mimi nashangaa sijui imekuwaje nikampenda. Nimejikuta nipo kwenye uhusiano naye na kwa kweli tunapendana sana.”
Mmoja wa wajukuu wa bibi huyo, Margaret Cheba, akizungumza na mwandishi wetu kuhusu tukio hilo alisema bibi yao amewadhalilisha sana na wanaona aibu kupita mitaani kwa kitendo cha kutembea na Hamad. “Hili jambo limetufedhehesha sana sisi wajukuu zake halafu hata kimila ni tatizo, hairuhusiwi kabisa. Mbaya zaidi, bibi yetu ni mgonjwa. Anasumbuliwa na moyo... sio wa kufanya kitendo kama kile kabisa na sisi ndiyo tunamsaidia lakini inashangaza polisi wametubadilikia kabisa,” alisema Cheba

FUMANIZI!!! KIGOGO AKAMWATWA AKIVUNJA AMRI YA SITA NA MWANAFUNZI BILA AIBU.......CHEKI HAPA
MZEE mmoja
kigogo wa biashara ya kuuza mbao jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alinaswa
kitandani ndani ya chumba akiwa na mrembo aliyedaiwa ni mwanafunzi wa shule
moja ya msingi Tegeta Wazo, Dar.Mfanyabiashara huyo aliyetajwa
kwa jina moja la Kyando, anasemekana amekuwa na ukaribu na denti huyo anayeitwa
Fatty kwa siku nyingi, kitu ambacho kiliwapa maswali baadhi ya majirani wa
nyumbani kwa msichana huyo.
Katika harakati za kuchunguza ukaribu
wa msichana huyo na mtu mzima huyo, mama mdogo wa binti aligundua kuwa wawili
hao wana ukaribu usiofaa.
Ikaelezwa kuwa, mama mdogo wa mwanafunzi huyo aliponyetishiwa ishu hiyo, aliandaa mtego unaofyatuka kwa kasi kuliko ule wa panya ili kumtia mikononi mzee huyo mpenda kukaa na watoto wa wenzake.
“Mtego mkali uliandaliwa, siku ya siku, ma mdogo huyo alijifanya anakwenda mbali na nyumbani, binti akaona dakika tisini za mchezo lazima aibuke kidedea wa mahaba, alimwita mwanaume huyo na kumkaribisha chumbani, kumbe arobaini zao zilikuwa zimetimia,” kilisema chanzo.

Ili kushika ushahidi mkononi, mama
mdogo wa binti huyo na wapambe wake walipiga picha za mnato na za video kisha
wakaanza kumuuliza maswali ‘mlalamikiwa’ ambaye inaaminika ni mume wa mtu.
Haikuelezwa wazi ni maswali ya aina gani aliyokuwa akiulizwa lakini inadaiwa yalihusu historia ya kujuana kwao.
Aidha, inadaiwa kuwa mama mdogo huyo alitaka kumtwanga ndoa ya mkeka mfanyabiashara huyo lakini chondechonde zake nyingi zilimwokoa na kuahidi kurejea siku inayofuata kwa ajili ya kukata mshiko wa fidia baada ya kuambiwa binti huyo bado anasoma na shuleni kulilipwa fedha nyingi.

Habari nyingine zinadai kuwa wawili
hao walifahamiana miezi kadhaa nyuma kupitia lifti ya gari ambayo mshitakiwa
alimpa mrembo huyo maeneo ya Boko, jijini Dar.
Labels:
Udaku
PICHA ZA UCHI..!VIDEO..!Serikali yatoa onyo kwa wanaume wanaowapiga picha za uchi wapenzi wao, ICHEKI HAPA
Serikali imesema haitavumilia mtu au kundi la watu wa
aina yoyote ambao watabainika kuendeleza vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa
kijinsia na kutaka jamii kutumia madawati ya jinsia katika vituo vya polisi
kuripoti matukio yote ya aina hiyo ili yadhibitiwe kabla ya kuleta
madhara makubwa ikiwemo watu kupoteza maisha.
Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya ndani Mh Dk Emanueli Nchimbi wakati wa uzinduzi wa dawati la jinsia pamoja na mpango kazi wa miaka mitatu unaaonyesha majukumu ya jeshi la polisi katika kuimaraisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Naye mkuu wa jeshi la polosi nchini IGP Saidi Mwema amesema tangu kuanza kufanyiwa majaribio mpango huo umeonyesha mafanikio makubwa na hivyo ameitaka jamii kujitokeza na kutumia dawati hilo.
Akizungumza katika hadhara hiyo mratibu mkazi wa umoja wa
mataifa Bw Aliberic Kacou amewataka viongozi kuhakikisha kuwa wanatumia nafasi
zao pamoja na sheria zilizopo kuhakisha kuwa wanawadhibiti wale wote ambao kila
mara wamekuwa wakifanya vitendo vya kikatili kwa makusudi.
-ITV
MAAJABU YA MUNGU!!... HUYU NDIYE MWANAUME MWENYE MOYO ULIO OTEA TUMBONI HUKO CHINA......MCHEKI HAPA
Ho
Zhiliang, 24, raia wa China amezaliwa huku moyo wake ukiwa unaota maeneo ya
tumboni kama unavyo ona kwenye picha. Kijana huyu ana subiri upasuaji ili
kuweza kurekebisha kiungo hicho na kukirudisha mahali kinapotakiwa kuwa.
Kweli
Mungu ni wa ajabu sana maana inasemekana watoto wengi wanao zaliwa na tatizo
hili hufa siku chache baada ya kuzaliwa lakini imekuwa tofauti kwa huyu kijana
ambaye ni kinyozi na ameamua kuishi maisha yake na hali hiyo hadi pale alipo
soma kwenye gazeti moja kwamba hali hiyo inaweza rekebishwa kwa opareshi ambayo
ndo anasubiria.
Labels:
Lifestyle & Fashion,
News
Tuesday, 26 November 2013
BEST FEMALE ACTRESS IN TANZANIA
Tanzanian Film Industry has many top female actress talented in movie career, Most of them being female, the listed are considered to be the best since 2007 in Tanzanian movie Industry known as “BONGO MOVIE”
Name: Irene Uwoya.
Best known for the movies of..
Question Mark, Apple,Safari,Zawadi Yangu, Innocent Case, Nyota Yangu, Last Card,
Doa la Ndoa, Ngumi ya Maria, Chupa Nyeusi, Kiapo, Eagle Eyes, Diversion of Love,
Fair Decision, Pretty Girl, Damu Moja, Shakira, Yolanda, Tanzanite.
Doa la Ndoa, Ngumi ya Maria, Chupa Nyeusi, Kiapo, Eagle Eyes, Diversion of Love,
Fair Decision, Pretty Girl, Damu Moja, Shakira, Yolanda, Tanzanite.
Name: Elizabeth Lulu Michael
Best known for the movies of..
Oxygen, Elizabeth Michael,House Boy, Ripple of Tears, Confusion,Ritazo, Family Disaster, Woman with Principal, Foolish Age.
Name: Wema Sepetu
Best known for the movies of..
House Boy, Crazy Tenant, Basilisa, The Diary, Lerato, Tafrani, White Maria, Sakata, Family Tears.
Name: Skyner Ally
Best known for the movies of..
What is It, Why I Did Love, I Hate My Birthday’, Kizungumkuti’, Unpredictable, Shahaada
Name: Yobnesh Yussuph aka Batulli
Best known for the movies of..
Kazi Yangu, Waves of Sorrow, Fungate,Get Out, The Glory of Ramadhan, My Fiance,Ripple of Tears, Machoz
Name: Jacky Wolper
Best known for the movies of..
After Death, Impossible,My Princess,Tikisa, Mahaba Niue, Pain for Pain P.F.P, Think Before,
Identity Card, Babylon, Before Wedding,I am Not Your Brother,Curse of Marriage, Ulimi, Mr.Nobody, Pusi na Paku, Lupepo Village, Hukumu ya Mande, Mtekaji, Chocolate, End of Evil, The Diplomat, My Intention, Time After Time, Chaguo Langu, Siri ya Moyo Wangu, God is Great, Saa4, Swadakta, Gaitan, The Impact,Mens Day Out, Dunia Nyingine, Determination, Aching Heart, Shoga Yangu, Mafisadi wa Mapenzi, All About Love, Eagle Eyes, Wrong Decision, Mtegoni, Fake Love, Life 2 Life, Mtumwa, Secretary, Last Minutes, Jozani.
Name: Nargis Mohamed
Best known for the movies of..
Magic House, Yellow Banana, Woman with Principal
Name: Irene Paul
Best known for the movies of..
Love & Power, Kibajaji, Kalunde, Fikra Zangu, Penzi la Giza, Love Me or Love Me Not,
I Hate My Birthday, The Shell, Handsome wa Kijiji
Name: Shamsa Ford
Best known for the movies of..
Zawadi Yangu, Babylon, Get Out, Dont Try, I Think I hate My Wife, Loreen,
Zawadi ya Birthday, Red Mzula, Mafisadi wa Mapenzi, Crazy Love, Saturday Morning
Name: Salma Jabu aka Nisha
Best known for the movies of..
Tikisa, Subiri Mama, Matilda, I am Lost, Pusi na Paku, Mchana wa Kiza,
Kashfa Macho Yangu, Red Cross
Name: Aunt Ezekiel
Best known for the movies of..
Pumba, Jungu la Urithi, Eyes on Me, Radio Presenter,Machozi Yangu, The Beauty Fools,
Kijogoo, Siku za Maajabu, Best Losers, Alice & Janel, I Hate My Birthday, Lost Souls,
Mens Day Out, Shoga Yangu, Lonely Heart, The Mask, Green Light, Sound of Death,Black Sunday,Taste of Love, Endless Love, Same Girl, The Village Pastor, Wicked Love,
The Cold Wind.
Name: Shilole
Best known for the movies of..
Chungu ya Nafsi, Barmaid, Macho Yangu, Kisasi cha Jessica, Mafisadi wa Mapenzi,
Talaka Yangu
Name: Kajala Masanja
Best known for the movies of..
House Girl & Boy, Dhuluma, Shortcut, Basilisa, Devil Kingdom
Name: Rose Ndauka
Best known for the movies of..
Waiting Soul, One Night, Fall in Love, Waves of Sorrow,Malaika,The Same Script,
The Specialist, Real Promise, Swahiba,Kwa Heshima Ya Penzi, Love Me or Love Me Not,
Jessica, Because of You, Ruben and Angel, The Diary, Solemba,
Bad Girl, Cut Off, Sound of Death, Why Did I Love, Mahabuba
Name: Warda Walid
Best known for the movies of..
Triple L, Nipende Monalisa, The Lost Adam
Name: Stella Premsigh
Best known for the movies of..
Sweet Liar.
Name: Monalisa
Best known for the movies of..
Dakika ya Mwisho, Chai Moto, 38 Weeks, Cellular, Girlfriend.
Labels:
Intertainment,
Lifestyle & Fashion
Subscribe to:
Posts (Atom)